Alvaro Morata na David Silva walikuwa miongoni mwa waliotikisa wavu viongozi wa Kundi G Uhispania walipolaza Liechtenstein 8-0 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

Baada ya kulaza Italia 3-0 Jumamosi, Uhispania walikuwa wanaongoza kwa 3-0 ndani ya dakika 16 mjini Vaduz kupitia mabao ya Sergio Ramos, Morata na Isco.
Kiungo wa kati wa Manchester City Silva aliongeza la nne kabla ya Iago Aspas kufanya mambo kuwa 5-0.
Iago alimsaidia Morata kufunga lake la pili kisha mwenyewe akajifungia bao lake kabla ya Max Goppel kujifunga dakika za mwisho na kukamilisha ushindi huo.
Iago Aspas and IscoHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionIago Aspas na Isco
Uhispania wanaongoza Kundi G wakiwa na alama tatu na wameongeza tofauti yao ya mabao hadi 29, mabao 17 zaidi ya Italia walio wa pili na ambao walilaza Israel 1-0 Jumanne.