Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameagiza viongozi wote waliotajwa katika ripoti ya uchunguzi dhidi ya madini ya almasi na tanzanite kujiuzulu mara moja kupisha uchunguzi.

Hata hivyo ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwa kamata mara moja wote waliotajwa katika kashfa hiyo ya madini.
George Simbachawene, Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) tayari amejiuzulu baada ya matamshi ya rais.
Ripoti za kamati zimewataja baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi,na Katibu mkuu wa wa Wizara ya Nishati na Madini
Magufuli amesema watanzania wanapaswa kuwa na uzalendo na kwamba mfumo utendaji wa madini unapaswa kurekebishwa ili na ufanisi kwa taifa.Kamati mbili za uchunguzi dhidi ya madini ya almasi na tanzanite imewasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Ikulu Dar es salaam.