Mchezaji wa tenis muingereza Dan Evans amefungiwa kwa mwaka mmoja kujihusisha na mchezo huo baada ya vipimo alivyochukuliwa kuonyesha kwamba anatumia Cocaine dawa zilizokataliwa michezoni.
Evans anasema alitumia dawa hizo kwa bahati mbaya.
Mchezaji huyo namba nne kwa ubora nchini Uingereza alipimwa katika michuano ya Barcelona Open April 24, na kuonekana kutumia dawa hizo, na adhabu hii itaanza tarehe hiyo ilipogunduliwa.
Kwa maana hiyo Evans mwenye miaka 27 atarejea uwanjani April 24, 2018.
Image captionEvans alifika hatua ya nne bora katika michuano ya Australian Open mwezi Januari
''Nitarejea tena katika mchezo niupendao, ninaamimi hilo,nashukuru kwa kila mmoja aliyeniunga mkono wakati huu mgumu.'' alisema Evans.
Tiyari alikuwa amefikia nafasi ya 41 duniani nwa kwa adhabu hii ataporomoka mpaka nafasi ya 108.
0 Comments