MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Marekani Donald Trump akisalimiana na wakaazi wa Puerto Rico
Rais wa Marekani Donald Trump amekimwagia sifa kitengo cha dharula na wafanyakazi wake walioko Puerto Rico kwa jinsi walivyo itikia wito wa kukabiliana na kimbunga Maria, ambacho kiliikumba ardhi hiyo yapata wiki ya pili sasa, kimbunga na tufani hiyo ilisababisha vifo vya watu kumi na sita na kuharibu maelfu ya makaazi.

Katika ziara yake ya kwanza katika wilaya hiyo iliyomo katika himaya ya Marekani tangu dhoruba hiyo ilipotukia, Trump aliweka utani kidogo katika mazungumzo yake juu ya gharama ya kurejesha maisha upya amesema kwamba ni sawa na kuitupa bajeti ya serikali yake kama mripuko.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Puerto Rico amesema kwamba wakaazi walio wengi bado wana hasira kwa serikali yao ya shirikisho kwa namna wanavyoshughulikia suala hilo.
Zaidi ya asilimia tisini na nane ya watu hawana nishati ya umeme na walio wengi zaidi hawana maji safi na salama ya kunywa.