Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa namba
maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.  Wanaoshuhudia kulia kwake ni Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu na  Mwenyekiti wa Bodi ya
mfuko huo, Godfrey Simbeye. Kushoto kwa Mhagama ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman
Jafo na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Khamis Mwinyimvua.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati)
akifurahia pamoja na viongozi wenzake  mara
baada ya uzinduzi huo.
 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 660 Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu.
 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akimkabidhi hundi ya sh. milioni
200 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ( kulia) kwa ajili ya ujenzi wa
kituo cha afya Mererani. 
 Mwenyekiti
wa bodi wa mfuko, Godfrey Simbeye akizungumza kabla ya uzinduzi wa namba hizo.
 Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko akizungumza kwenye tukio hilo.
 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akitoa hotuba katika tukio hilo.
 Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akisisitiza jambo baada ya kukabidhiwa
hundi yake.
 Washiriki
wakifuatilia mkutano huo.
 Mawaziri
wakiangalia namna ya kutuma fedha kwa kutumia namba  0684909090 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa
udhamini wa kudhibiti Ukimwi. Aliyesimama ni Mkuu wa kitengo cha sheria wa
TACAIDS, Elizabeth Kaganda.
 Waziri
Mhagama (katikati) akiwa katika picha na viongozi wengine.
 Mawaziri wakiagana mara baada ya kumaliza uzinduzi wa tukio hilo.

Picha na Philemon Solomon
.....

Na Julian Msacky-Nchi yangu Blog.

TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), imezindua rasmi
namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.

Uzinduzi huo umefanyika Dar es Salaam Oktoba 21, 2017 na kuzinduliwa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Mhagama.
Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko huo kuwa ni
0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa kuchangia ili fedha
itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi. 

"Leo ni siku maalumu kwa nchi yetu...inaonesha
tumeanza kujitegemea kupitia mfuko huu wa udhamini katika mapambano dhidi ya
VVU na Ukimwi," alisema.
Waziri alisema mfuko huo umeanzishwa kwa Sheria Namba 6 ya Mwaka
2015 na utakuwa unachangiwa na Watanzania wenyewe.

"Huu ni mfuko wa umma na tunabeba jukumu hilo kama
Serikali na lengo kuu ni kuwahudumia Watu wenye maambukizi,"
alibainisha.

Alisema fedha za mfuko huo zitatumika kununua dawa za
septrine ambazo ni maalumu kwa ajili ya kufubaza Virusi Vya Ukimwi na
zitatolewa bure.