Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati wa mahojiano yasiyo ya kawaida tangu aondoke madarakani mwezi Januari.
Alionya kuwa vitendo kama hivyo vinachanganya uelewa wa watu katika masuala magumu na kusambaza uvumi.
Mrithi wake Donald Trump ni mtumiaji mkubwa wa Twitter lakini Obama hakumtaja jina.
Obama alihojiwa na Prince Harry katika BBC Radio 4.
Obama alisema wale walio katika nyadhifa za uongozi wanastahili kuwa waangalifu wakati wanaandika katika mitandao.
Alielezea wasi wasi kuhusu siku za usoni ambapo ukweli utapotoshwa na watu watakuwa wakisema, watakuwa wakisoma na kusikiliza vitu ambavyo vitakuwa vikiridhisha maoni yao.
0 Comments