WATU
11 wamefariki Dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya
gari aina ya hiace kugongana na malori matatu iliyotokea mnamo majira ya
saa tano usiku wa kuamkia leo,katika kijiji cha Mubigera kata ya
Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera ,wakati wakisafiri kutoka
wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga.




Mganga
mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha
kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati
ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya
kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Dr Sebuyoya amewataja
waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard
Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25)
na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti
waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa
hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw
Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni
ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo
kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na
tingo wake ni miongoni mwa waliofariki

Bw Kayuki amesema hiece
hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda
kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103
DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa
uchunguzi zaidi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino
Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni
pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na
taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu
waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika