Wanaume watatu nchini Zambia wamelazwa kwa makosa katika wadi ya wagonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, ameiambia BBC kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili.
''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa''
Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hiko cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza bwana Kasolo.
Wanaume hao watatu wanatoka katika mji mdogo wa katete, na si wagonjwa wa kipindupindu bali walikunywa dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya tendo la ndoa inayojulikana kama Mvubwe.
Ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka mwaka jana ulisababisha vifo vya watu takribani 70, kusini mwa Afrika.
Rais Edgar Lungu mwezi uliopita, alitoa agizo kwa jeshi la Zambia kusafisha maeneo ya masoko na kuondoa uchafu ambao ndio saabu ya kipindupindu.
|
0 Comments