Marehemu Jaji Mstaafu Robert Kisanga.
Jaji Mstaafu Robert Kisanga amefariki dunia leo katika Hospitali ya Regence ya Jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa.
Taarifa za kifo cha Jaji Kisanga zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa John Kahyoza. Mbali na Mahakama ya Rufaa, Marehemu Jaji Robert Kisanga alifanya kazi Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Jaji Robert Kisanga aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kabla ya kustaafu mwaka 2008.