Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano wa masuala ya kiuchumi World Economic Forum WEF unaofanyika mjini Davos , Uswizi.

Bw Kagame atakuwa kiongozi wa pekee wa bara Afrika anayetarajiwa kukutana na Trump kulingana na ratiba iliyotolewa na mshauri wa masuala ya kiusalama wa Marekani H.R McMaster.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa unajiri huku kukiwa na malalamishi makubwa dhidi ya Trump ambaye aliyataja mataifa ya Afrika kuwa ''machafu" au ya "mabwege" katika mkutano wa kuzungumzia sera za uhamiaji.
Baadaye alikana madai hayo.
Mkutano wa rais Trump na Kagame, ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika utaimarisha uhusiano wa Afrika na Marekani na kuzungumzia masuala muhimu ikiwemo biashara na usalama.
Paul Kagame ndio mwenyekiti wa sasa wa muungano wa Afrika
Image captionRais wa Rwanda Paul Kagame kukutana na rais Trump katika mkutano wa kiuchumi wa World economic Forum mjini Davos
Muungano wa Afrika umemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa matamshi yake ya kukera.
Bwana Trump pia anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na rais wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Davos.
''Katika mikutano yake yote, raia huyo anatumai kuimarisha fursa za kujenga uchumi miongoni mwa raia wa Marekani," alisema Bw McMaster.