Ukamhitaji mkunga jijini Nairobi, Kenya na unaweza kupata mgeni kutoka kwa Margaret Wairimu Maina.
Margaret hutembea kwa miguu huku akiwa amebeba begi lake mgongoni utadhani ni mwanaanga.
Begi hilo huwa na vifaa vya hali ya juu vya kiteknologia vya kupima hali ya afya ya mama na mtoto.
Begi hilo ambalo hulibeba mgongoni huwa na kifaa cha kumpia mtoto jinsi moyo unavyopiga, skrini ya Ultrasound, mwanga unaotumiwa wakati wa matibabu unaotumia miali ya jua, kipima joto cha masikioni na vitu vingi vya kiafya vinavyohusishwa na uja uzito.
Kazi yake imekuwa yenye changamoto nyingi sana hasa kwake yeye kama mfanyikazi wa kujitolea wa afya.
"Licha ya kwamba begi hilo lina uzito wa kilo tano pekee, bado ni mzigo mzito kwani mimi huzunguka mara mbili kwa wiki," amesema Margret.
"Bi Margret hutembelea karibu nyumba 120 katika eneo hilo na huweza wanazuru watu 20 kwa siku kati ya saa sita mchana na saa kumi alasiri.
''Nina watoto wawili, mmoja ana umri wa miaka 5 na mwengine 11.''
"Uja uzito wangu haukukumbwa na shida yoyote kwa sababu nilianza kutembelea kliniki ya kupokea mafunzo ya kabla ya kujifungua mapema miezi miwili baada ya kupata mimba na pia wakati wa kujifungua nilikuwa na mtu mwenye uzoefu wakati huo.
"Si wanawake wengi nchini Kenya ambao hubahatika kama nilivyobahatika mimi.
Nchini Kenya, tofauti na mataifa mengine ya bara Afrika kama vile Ethiopia, huduma ya wakati wa uja uzito hailipwi na serikali au mamlaka ya mitaa.
Margaret hufanya kazi katika zahanati ya Kiambu ya Community Life Centre iliyoko Kaskazini mwa Nairobi, ambapo wafanyikazi wa umma huwapeleka wagonjwa ambao huhitaji msaada wa kimatibabu.
"Kwa kiwango kikubwa barani Afrika, watu kama Margaret ambao hawalipwi chochote kwa kazi zao za kujitolea na hawana mafunzo maalum ama hata vifaa vya kutumia wanapotoa huduma," amesema mkurugenzi mkuu wa Philips Africa, Jasper Weasterink ambao walitengeneza begi hilo la mgongoni.
''Kwa miaka mingi, tumekuwa tukiangazia masuala ya afya ya mama na mtoto nchini Afrika.''
Philips inaboresha vituo vya matibabu zaidi ili kuwasaidia wafanyakazi wa afya na wakunga kuwahami na vifaa vya kiteknolojia na begi hilo la kiteknolojia.
''Lengo letu kubwa ni kuanzisha mfumo huo kila mahali barani Afrika ili kuboresha huduma ya kwanza,'' amesema Bw Westerink.
Hata hivyo , kwa upande mwingine wa Nairobi kuna mtaa wa Kibera.
Ni kitongoji duni kikubwa barani Afrika na ni makao ya watu 500,000 na hata inakadiriwa kuwa mtaa huo una uwezo wa kuwahifadhi watu milioni mbili.
Kibera haina huduma nzuri ya maji taka au maji safi - njia katika mtaa huo ni panda ambapo magari ya kuwabebea wagonjwa hayana uwezo wa kuingia ndani mtaani.
Na kile kitu ambacho kinauwezo ni mkokoteni (ruukwama) ambao unawekwa king'ora cha samawati kilichowekwa kwenye pahala pa kukamatia unapouburura.
Wagonjwa huwekwa kwenye mkokoteni huo na wenye bahati hupelekwa kwenye zahanati ya jamii
Lakini katika mji wa Mandera, uliopo katika mpaka wa Kenya na Ethiopia, wanawake wajawazito hawana hataa mkokoteni wa wa kuwabebea wagonjwa.
Inachukua siku mbili kufika katika mji huo kwa kutumia barabara kutoka Nairobi na idadi ya vifo vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano ni kubwa zaidi ulimwenguni huku vifo 4,000 vikiripotiwa kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.
Huduma ya usafiri ni ghali huko na njia ya pekee ni kutumia ngamia kwa wanawake wajawazito.
Na ni jambo la kushangaza wakati wanapofika kwa daktari, maisha ya mama mjamzito yako hatarini, na pia kuna hatari ya kumpoteza mtoto wake pia.
Kliniki mpya ilianzishwa katika eneo hilo mwaka jana kupitia ushirikiano kati ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watu (UNFPA), serikali ya kaunti ya Mandera na kampuni ya Philips
"Vifo vya kina mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano katika kaunti sita ambazo hazifikiki kwa urahisi Kenya huchangia karibu asilimia 50 ya vifo vya aina hiyo kote nchini Kenya. Na tunataka kukomesha vifo hivyo kwa kutumia vituo kama hivyo," anasema Dkt Ademola Olajide wa UNFPA.
0 Comments