Inaonekana kwamba Alexis Sanchez alipanga kuelekea Manchester City lakini Manchester United ikawa na mipango mengine.
Katika usajili wa mchezaji nyota kutoka kwa mpinzani mkubwa, kujiunga kwa Sanchez katika klabu ya United kunafanana na Carlos Tevez kujiunga na Manchester City kufuatia kuondoka kwake katika klabu ya Red Devils mwaka 2009 -hatua ilioifanya City kuweka bango katika mji wa Manchester ikimkaribisha mchezaji huyo.
Uhamisho wa Robin Van Persie 2012 kutoka Arsenal ambapo City ilikuwa inamuhitaji ambapo mkataba huo ulikuwa wa kubaini ni klabu gani itashinda ligi.
Ni vipi Sanchez alienda Man United badala ya Manchester City? ni wapi atakapochezeshwa? Na je Arsenal ambayo imempokea Henrikh Mkhitaryan ikiwa ni mojawapo ya makubaliano itafanya nini?
Ilikuwaje Alexis Sanchez akaelekea Man Utd?
Iwapo klabu ya Manchester City ingemchukua mchezaji huyo mwezi Agosti iliopita, isingefikia uamuzi wa yeye kuelekea United.
Ijapokuwa dau la uhamisho wa £60m katika siku ya mwisho ya uhamisho wa msimu uliopita liliafikia kiwango kilichotakiwa na Arsenal, halikutoa muda wa kutosha kwa Arsenal kusukuma uhamisho wa Thomas Lemar kutoka Monaco.
Mshambuliaji huyo wa Chile alisalia akisubiri huku City ikisubiri kwa ujasiri lakini United ilisubiri na baadaye ikamnyakua.
Kwa uwazi, Pep Guardiola na uongozi wa klabu hiyo alijua kwamba usajili wa Sanchez utazua maswala makali ndani ya kikosi cha Manchester City katikati ya msimu.
Mshahara mkubwa unaohusishwa na ununuzi wa mchezaji kama Sanchez ulifanya mambo kuwa magumu.
Mchezaji huyo alitarajiwa kupokea mshahara mkubwa kumshinda Kevin de Bruyne wakati mshahara wake utakapoongezwa.
Huku kukiwa na lengo la kushinda taji la ligi mbali na matumaini ya kushinda kila taji ikiwemo lile la vilabu bingwa kwa mara ya kwanza ,City haikuwa tayari kufanya hivyo na kuhatarisha uwepo wa kundi la wachezaji ambalo limefanya vyema katika kipindi cha kwanza cha msimu.
United, iliokuwa ikisaka wachezaji kufuatia tamko la Jose Mourinho la hivi karibuni kwamba £300m
Kwa Mourinho, maswala ya kikosi chake sio muhimu zaidi ya kuunda kikosi kitakachoshinda mataji.
Licha ya kushinda taji la EFL na lile la Yuropa katika msimu wake wa kwanza ,Mourinho anajua kwamba iwapo unataka kushinda mataji makubwa basi utahitaji wachezaji wazuri na Sanchez ni mmoja wa wachezaji hao.
Waliuliza bei, waliambiwa ada ya ajenti wake na kuanzisha mpango wa kumnunua.
Duru zilizopo karibu na mkataba huo zinasema kuwa ungeafikiwa hata bila ya kuhusishwa kwa Mkhitaryan. Hatutajua ukweli wa hilo.
Lakini kupitia Mkhitaryan, United walikuwa na mchezaji muhimu wa ziada ambaye Arsenal walikuwa wanammezea mate. City hawakuwa na nyongeza kama hiyo katika mpango wake wa kumnunua mchezaji huyo .
Katikati ya msimu ,klabu iliokuwa ikimtaka Sanchez ilifanikiwa kumnunua mchezaji huyo. Baada ya hilo ilikuwa ni ubabe wa kifedha.
Kama Mourinho alivyonukuliwa akisema baada ya Liverpool kulipa £75m kumnunua beki Virgil van Dijk: "Iwapo unamtaka mchezaji ni lazima ugharamike .
Mourinho amemsajili mchezaji ambaye Guardiola angependelea kuwa naye katika kikosi cha Manchester City - lakini iwapo amempiku mwenzake ni swala jingine
Kuna hisia kwamba duniani mbali na maswala magumu ya mipango ambayo huandamana na mikataba mikubwa , Sanchez angependelea City badala ya United akiwa na fursa ya kufanya kazi na Guardiola tena baada ya kufanya kazi pamoja wakiwa Barcelona.
Iwapo City ilikuwa na mpango wa kifedha kupitisha mkataba huo , Sanchez angekuwa mchezaji wa uwanja wa Etihad badala ya Old Trafford.
Uamuzi wa mwisho wa iwapo Mourinho amefanya mapinduzi dhidi ya Guardiola utafanywa katika matokeo na uwanjani.
Mourinho na United wamemsajili mchezaji mzuri zaidi duniani , mtu ambaye anaheshimiwa sana na Guardiola na hakuna tashwishi yoyote kwamba ana uwezo wa kuwa na athari kubwa katika uwanja wa Old Trafford.
Na hilo litaonekana kua ushindi mkubwa kwa mourinho na United.
Iwapo atashirikishwa katika safu ya mashambulizi ya Mourinho huenda akaisadia United kuikaribia City katika jedwali la ligi na hata kuipita katika siku za usoni.
Kwa sasa, hatahivyo, mbali na kumpiku Mourinho ,ni wazi kwamba United iko tayari kutumia kiwango chochote cha fedha zaidi ya City kununua wachezaji inaowataka
Ni eneo gani atachezeshwa uwanjani Old Trafford?
Sanchez ni mchezaji anayezunguka uwanja mzima , anaweza kucheza kushoto, anaweza kucheza kulia na anaweza kucheza katikati kama mshambuliaji na hata namba kumi.
Ni usajili mzuri uliofanywa na United. Una mchezaji anayewza kucheza maeneo manne, kwa hivyo pale ambapo amezoea inategemea hali ya kiwango cha washambuliaji wengine na kile ambacho Mourinho anataka kufanya katika mechi tofauti kwa sababu tunajua anapenda kuwazungusha wachezaji wake.
Kitu ambacho United imekuwa ikikosa , ijapokuwa Jesse Lingard amefanya vyema ni kumsaidia Lukaku kutoka nyuma na kumletea mipira.
Hio ndio nafasi ambayo ninaweza kuona Sanchez akichezeshwa ,karibu na nyuma ya Lukaku akiwa mchezaji huru nambari 10 mbele ya Paul Pogba na Nemanja Matic.
Upande wa kushoto wa United ni nafasi nyengine ambayo anaweza kiucheza- licha ya kuwa yeye hucheza kwa mguu wa kulia ambapo hupenda kushoto na kukata na kuingia ndani kutoka hapo.
Lakini mchezo wa Anthony Martial na Jesse Lingard umeimarika hivyobasi huenda upande wa kulia wa safu ya mashambulizo ndiko ambapo huenda akachezeshwa. hatahivyo haijalishi.
Tunajua kwamba Sanchez anaweza kucheza vyema popote katika safu ya mashambulio na tunajua alivyo mzuri kutokana na vile tulivyomuona katika jezi ya Arsenal.
Wakati unapokuwa na talanta kama yake unataka apewe mpira hususan katika eneo la mashambulizi. Sidhani kwamba unaweza kumfunza mchezaji kama yeye .
Ni kweli unaweza kumweka katika maeneo ambayo unapoteza mipira, ataingiana katika mfumo wa mchezo wa United kwa njia hiyo -na wanapofanya mashambulizi basi wanafaa kumtumia.
Je City wana wasiwasi kwa kumkosa Sanchez?
Sanchez angeingiana vyema na mchezo wa City.
Najua angependelea kwenda huko iwapo City ingeafikia kiwango cha dau la United lakini tayari walikuwa wameamua kwamba hawawezi kumnunua mchezaji huyo.
Walikuwa wanamuhitaji kwa sababu walikuwa wamemnyatia kwa miaka kadhaa na walikaribia kumsajili mwisho wa msimu uliopita.
Naelewa kwa nini, kwa sababu ni mchezaji ambaye wanamtaka na angeingiana vyema na mfumo wa mchezo wao katika maeneo tofauti sawa na ambavyo atacheza akiwa Man United.
Ni mchezaji anayependwa na Guardiola kwa sababu anapenda kusukuma- kama ulimtazama akiwa Arsenal utaona ni mchezaji ambaye anapenda kutoa shinikizo ama changamoto kwa wapinzani akiwafukuza na kujaribu kuwanyang'anya mpira haraka iwezekanavyo.
Akiwa na umri wa miaka 29 ana miaka minne ama hata mitano ya kucheza mbele yake na ukitazama msimu huu basi angeimarisha City wakati inapofukuzia mataji manne.
Huku Gabriel Jesus akiwa amejeruhiwa tangu kuanza kwa mwaka huu , Sergio Aguero ndio mshambuliaji wa pekee aliye katika hali nzuri na Guardiola alitaka mchezaji mwengine.
Hamu ya City katika kumsajili Sanchez imeibua uvumi kuhusu hatma ya Aguero kwa sababu ijapokuwa anafunga magoli mengi kuna swali la iwapo anafanya kile Guardiola anachopenda miongoni mwa wachezaji wake .
Aguero anafanya bidii ikiwa hana mpira zaidi ya alivyokuwa, lakini je anatoa shinikizo ya kutosha, ama hufukuzia mpira kwa kile Guardiola anachotaka?
Sanchez bila shaka yeye hufanya hivyo. Pengine City ina chaguo jingine kwa sababu wanahitaji mshambuliaji mwengine.
Mkhitaryan - Kuvunjika kwa uaminifu
BBC Sport's Simon Stone
Kuondoka kwa Mkhitaryan katika klabu ya United baada ya miezi 18 akiwacha hasira ya mashabiki ya Old Traford ambao hawakuona mchezo mzuri wa raia huyo wa kwanza Muarmenia.
Mwezi Julai 2016 mambo yalionekana kuwa tofauti.
Ajenti wa Mkhitaryan Mino Raiola asiyekosa utata aliibembeleza Borussia Dortmund kumuuza kiungo wao muhimu. Aligharimu £30m na kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Mourinho.
Mashabiki wa United walionyeshwa kionjo cha matarajio yao wakati wa mechi ya kwanza ya kiungo huyo ,anbayo ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Wigan .
Na miezi miwili baadaye matarajio ya wengi yaliangukia patupu.
Baada ya kuchezeshwa mara tatu kama mchezaji wa ziada ,Mkhitaryan alianzishwa dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Old Trafford .
Kwa dakika 40 wenyeji walitawaliwa na wageni wao.
Wachezaji wa United walishindwa kujizatiti lakini baadaye ikawa ni Mkhitaryani ambaye hakurudi uwanjani katika kipindi cha pili.
Hakuanzishwa mechi nyengine ya ligi ya Uingereza kwa miezi mitatu.
Na kweli ijapokuwa kuna wakati ambapo Mkhitaryan aliweza kumvutia mkufunzi wake -alifunga katika mechi ya ushindi ya fainali katika kombe la Yuropa dhidi ya Ajax na hakuweza kuimarika tena.
Mchezo mwengine wa kiwango cha chini wa Mkhitaryan ulikuwa dhidi ya Chelsea mnamo tarehe 5 Novemba ambao ulipiga msumari wa mwisho katika hatma ya mchezaji huyo.
Kuvunjika kwa uaminifu kati yake na Mourinho hakukuweza kuimarishwa tena.
Mkhitaryan alianzishwa mechi moja ya ligi ya Uingereza. Katika mechi yake ya mwisho katika kombe la FA dhidi ya Derby, alionekana kana kwamba anazuiliwa kila aliposhika mpira.
Wakati alipotolewa usiku huo ilionekana kama kitendo cha kumuhurumia. Akiwa katika kiwango cha juu cha mchezo, Mkhitaryan ana kasi, ni jasiri akiwa na mpira katika miguu yake ana uwezo wa kudhibiti mpira na anatoa pasi murua.
Kwa sasa uwezo bado upo lakini ujasiri umepotea. Changamoto ya mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger kumuimarisha Mkhitaryan hadi alivyokuwa -kwa sababu kwa wale ambao wamemtazama akicheza Manchester United , wazo la Mkhitaryan kuwa sawa na Sanchez litategemea muendelezo wake.
Je hatua hii inaiwacha wapi Arsenal?
BBC Sport's David Ornstein
Arsenal ingemuuza Sanchez mwisho wa msimu uliopita iwapo wangefanikiwa kumsajili mrithi wake, hatua inayoonyesha kibinafsi kuwa wamekubali kuendelea na maisha bila mshambuliaji huyo wa Chile .
Hivyobasi kuondoka kwake hakukushangaza.
Masaibu ya kupoteza mchezaji mzuri hatahivyo hupunguzwa na ukweli kwamba Sanchez alishindwa kuonyesha mchezo mzuri , nusu ya kipindi cha kwanza cha msimu huu kwa kuwa hakuonyesha takwimu nzuri , hakuwa na ushawishi wowote na alikuwa tayari kuondoka.
Mpango wa Arsenal wa kukataa dau la uhamisho wa £60m kutoka kwa City na kumwacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kukamilisha mwaka wake wa mwisho katika kandarasi yake kwa lengo la kuwa atang'ara uwanjani uliambulia patupu.
Lakini kupitia Mkhitaryan Arsenal ina mchezaji ambaye imekuwa ikimsaka na wakamkosa kwa ncha ya ukucha 2016.
Mchezaji huyo wa Armenia anaingiliana na mchezo wao, ana umri mdogo ikilinganishwa na Sanchez alikuwa na thamani kubwa zaidi ya mchezaji huyo na anafurahia kuwa Emirates.
Hili ni tatizo ambalo The Gunners hawangejiingiza, ijapokuwa tatizo hilo lingekuwa baya zaidi iwapo Sanchez angeondoka bure mwisho wa msimu.
Na iwapo Mkhitaryan atachangia kuimarisha klabu hiyo hatua mabyo inadhani itaipigajeki katika kuwania mataji, basi usajili wake utaonekana kuwa mzuri.
0 Comments