Waombolezaji
wakiwa wamebeba  jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester
Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018.



 Marehemu Lulu  Sylvester Mattunda Lema.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


 Familia katika picha ya pamoja eneo la Korogwe Bararara ya Tanga


 




Waombolezaji wakiwa nyumbani hapo
 Sylvester
Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake
mara
baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji
cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi, Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya
Hai kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika Leo  Saa Nane Mchana,
Januari 26, 2018 katika makaburi ya familia yaliyopo eneo hilo

 Mwinjilisti wa Usharika wa Nronga, Donald Lema akizungumza  jambo baada ya mwili wa  marehemu, Lulu Sylvester
Mattunda Lema
ulipowasili katika
Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,
Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro  Januari 25, 2018 kwa taratibu za mazishi
yanayofanyika leo  Ijumaa Januari 26, 2018 saa Nane Mchana, katika makaburi
ya familia yaliyopo eneo hilo, ambapo Lema alisema, "Katika mtihani huu ndugu yangu Sylvester,umeshinda katika ile ahadi uliyotamka ni kifo ndicho kitakacho tutenganisha mimi na wewe Lulu,hivyo ahadi hiyo umeitimiza, Profesa Lema
pamoja na ndugu zako wote nachukua nafasi ya kuwapeni pole sana na Mungu akawatie nguvu, huyo aliyekufa maisha yake yamekwisha aliyebaki ndiye ameumia zaidi,wapo ndugu zetu waliokuwa Dar es Salaam ambao katika msiba huu walishughulika kufa kupona wahakikishe jambo hili limewezekana kama hivi lilivyowezekana, wapendwa niseme nivile tunauona msiba tukiusikia kwa mwingine, tumeona mwili umetufikia nyumbani,kutokana na msiba huu kuna watu
wanashughulika kwa kujitolea kwa hali na mali, wapo wanaotoa matangazo wapo wanaofanya hili na lile kuhakikisha jambo linakwenda vizuri na wapo waliojitoa kwa hali na mali ,na kwa wale waliotoka Dar es Sallam na kwa wale waliotoka ndani na nje ya nchi naomba

kuwashukuru sana kwaniaba ya ushirika wa Nronga kwa kufanya juhudi zote kuuleta mwili wa mpendwa hapa nyumba pia napenda kuwaambia mumtie moyo ndugu yenu pamoja na watoto na mumtegemee Mungu Kwa mioyo yenu yote, huu mwaka ni mwaka wa marejesho, atarejesha amani
pasipo amani, atarejesha baraka pasipo baraka, atarejesha afya mahali  afya imetoweka na huu mwaka nimzuri sana kwa anaemtegemea Mungu.