Raia wa Zimbabwe wanaoishi kwenye mji mkuu wa Namibia Windhoek, wanasema wameona aibu baada ya wao kulipishwa na ubalozi wa Zimbabwe nchini humo ili kwenda kumuona rasi Emmerson Mnangagwa.
Mtandao wa habari wa Namibia The Villager, ulisema kuwa wenyeji na raia wa Zimbabwe walilipa dola 16 ili kupata kiti kwenye hoteli ya Windhoek's upmarket Safari hotel kuweza kusikiliza hotuba yake.
Mtandao huo ulisema kuwa ubalozi wa Zimbambwe ulipeleka viti 300 katika eneo ambapo Bw Mnangawa alitarajiwa kuhutupia wanyeji wa raia wa Zimbabwe.
Watu kadha waliokuwa wamekasirika walisema walizuiwa kuingia.
"Tuliambiwa tulipe lakini baadhi yetu tulizuiwa. Wengine hawakuja na wakati tuliomba kama tutaingia kwa niaba yao waikataa. Tukipiga kura hatulipi, lakini kumuona rais tunalipa."
Mwishowe wale walioingia ni wale waliweza kulipa. Inaashiria jinsi ubalozi umekubwa na uhaba wa pesa.
|
0 Comments