|
MWENYEKITI Mwenza wa Taasisi ya Wanyamapori Afrika (AWF), Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini Tanzania, Benjamin Mkapa alisema, mara nyingi viongozi barani humo wanafanya uamuzi wenye athari hasi kwa urithi wa asili kwa kuwa hawana mitazamo na dhamira ya hifadhi.
Mkapa aliyasema hayo hivi karibuni akiwa eneo la Kinigi wilayani Musanze, Rwanda wakati AWF ikiikabidhi ardhi Hifadhi ya Taifa ya Volcano (VNP) ili kuongeza eneo la kuhifadhi sokwe wa mlimani.
Ameipongeza dhamira thabiti ya Rwanda kwenye uhifadhi. “Kama Mwenyekiti Mwenza wa AWF najivunia kutoa hii ardhi kwa Serikali ambayo imeonesha dhamira kubwa na uongozi kwenye uhifadhi,” alisema.
Katika tukio hilo, Rais wa AWF, Kaddu Sebunya alimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB), Clare Akamanzi mfano wa hati miliki ya ardhi. Sebunya alisema Rwanda imeonesha kuwa ni kiongozi kwenye suala la hifadhi kutokana na mafanikio makubwa kwenye kuongeza idadi ya sokwe ndiyo maana taasisi hiyo imejitolea ardhi kuongeza eneo la makazi ya wanyama hao.
Eneo hilo la hekta 27.8 litatumika kwa ajili ya mradi wa sokwe wa milimani, unaotekelezwa kwenye hifadhi ya Volcano. AWF imenunua eneo hilo kwa kusaidiwa na taasisi ya Annenburg ili lijumuishwe kwenye hifadhi hiyo yawe makazi ya sokwe
0 Comments