Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza akiongea na maafisa watendaji wa wilaya ya kilolo kwa lengo la kuhimiza ufanyaji kazi wao kwa kutatua changamoto za wananchi na hatimaye wapate maendeleo
pichani ni baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji,kata na tarafa waliohudhuria kikao hicho cha mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza




Na Fredy Mgunda, Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza amewataka watendaji wote wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mihemuko
ya kisiasa kwa kuwa linarudisha maendeleo nyuma.
 

Onyo hilo limetolewa wakati wa
kikao na maafisa watendaji wa wilaya ya Kilolo,Masenza alisema kuwa imebuka
tabia ya viongozi wa serikali kujihusisha na siasa wakati wa utendaji wao wa
kazi hivyo kuanzia saizi zitaki kusikia siasa wakati wa kazi.



“Haiwezekani kila siku mnafanya
siasa tu huko vijijini badala ya kutengeneza mpango kazi wa kimaendeleo ambao
utakuwa na faida kwa taifa na wananchi wote hivyo kuanzia leo sitaki kusikia
tena hiyo tabia” alisema Masenza



Masenza alisema serikali ya
awamu ya tano inataka watu wafanye kazi hivyo wakati siasa hakuna tena kama
kuna viongozi wanataka siasa wasubili wakati ukifika watafanya hizo siasa.



“Jamani rais wetu ameshasema
kuwa huu sio wakati wa porojo za kisiasa huko makazini hivyo mnapaswa kufanya
kazi na sio kupiga siasa fanyeni kazi kwa nguvu zote kuhakikisha mnatatua kero
za wananchi katika maeneo yenu husika” alisema Masenza



Masenza alisema kama kuna
mtendaji wa serikali anataka kufanya kazi za kisiasa basi hana budi kuachia
nafasi yake ya kazi ili akaendelee kufanya kazi ya siasa na nafasi yake
itajazwa na viongozi ambao wapo tayari kufanya kazi na serikali ya awamu ya
tano.



Aidha Masenza aliwaagiza
wakurugenzi wote mkoani Iringa kuwachukulia hatua za kisheria mara moja
viongozi wa serikali watakuwa wanajishughulisha na maswala ya kisiasa la sivyo
wao ndio watachukuliwa hatua kwa kufuata miongozo ya kiserikali inavyoagiza.



“ wakurugenzi mnawajua sana
hawa watendaji hivyo ni lazima muwadhibiti kufanya siasa wakati wa kazi na
mnatakiwa kuwa wakali pindi mtakapogundua kuwa wanafanya siasa makazini”
alisema Masenza



Naye katibu tawala wa mkoa wa
Iringa Wamoja Ayubu alisema kuwa ameshatoa walaka unaonyesha majukumu ya
watendaji wa serikali hivyo hategemee kuona kiongozi wa serikali akifanya siasa
kazini.



“Jamani nimetuma na kuwa walaka
wa majukumu yenu hivyo sitegemie mnakiuka la sivyo nitaanza kuwa sughulikia
kiongozi mmoja mmoja ili nikomeshe tatizo la siasa makazini” alisema Ayubu



Ayubu aliwataka makatibu wa
wilaya kufanya kazi kwa kufuata miongozo ya serikali la sivyo serikali
haitafikia malengo ya kuleta maendeleo kwa wananchi kama ambavyo wamejipangia
hivyo inapaswa  kila mmoja anafanye
majukumu yake kikamilifu ili kutimiza malengo ya serikali.



“Rais wa awamu ya tano DR John
Pombe Magufuli hataki tufanye kazi kimazoea kama ambavyo ili kuwa awali saizi
ni kazi tu hivyo ni lazima kufanya hivyo” alisema Ayubu