Shahidi mmoja ameielezea BBC aliyoshuhudia katika mkasa wa kuogofya wakati wanaume waliojihami kwa bunduki walipoivamia hoteli ya Intercontinental siku ya Jumamosi.

Mwanamume huyo ambaye hakutajwa jina kutokana na sababu za kiusalama, amesema aliponea shambulio hilo baada ya kusema kuwa yeye ni raia wa Afghanistan. "Wako wapi wageni?" walipiga kelele wakiuliza.
Raia 14 wa nchi za kigeni wamethibitishwa kuuawa pamoja na wanne wa Afghanistan.
Waziri wa mambo ya ndani amesema uamzui wa kukabidhi usalama kwa kampuni ya kibinfasi ulikuwa makosa.
Ni ishara ya hivi karibuni ya ghasia zinazoendelea kushudiwa nchini Afghanistan.
Usiku kucha, vikosi maalum vilipambana kuidhibiti hoteli hiyo.
Zaidi ya watu 150, wakiwemo wageni, walikuwemo ndani ya hoteli hiyo Jumamosi jioni wakati washambuliaji waliojihami kwa bunduki walipoivamia hoteli hiyo na kuanza kufyetuwa risasi.
Televisheni nchini humo zimewaonyesha wageni wakishuka kutoka orofani kwa kutumia matandiko, waliyoyafunga kwenye roshani na kukwepa.
Picha ya maktaba: The Intercontinental Hotel, picha iliyopigwa Januari 2016Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPicha ya maktaba: The Intercontinental Hotel, picha iliyopigwa Januari 2016
Moshi mkubwa ulitanda usiku angani, ikiwa ni baada ya sehemu ya jengo hilo kuteketezwa moto.
Hoteli hiyo ya Intercontinental ni mojawapo ya majengo makuu ya mji wa Kabul.
Hutumika sana na wageni wa nchi za nje, wanasiasa nchini, hutumika pia kuandaa shrehe za harusi na mikutano.
Ni eneo la wazi linaloweza kulengwa na wanamgambo na lilishambuliwana wapiganaji wa Taliban miaka 7 iliyopita.
Ramani ya Afghanistan
Image captionRamani ya Afghanistan
Lakini shambulio hili la sasa lililodumu kwa muda mrefu na linaloonekana kuwa gumu, linajiri katika wakati ambapo kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu kudorora kwa usalama katika mji mkuu huo, na litazusha maswali kuhusu vipi usalama wa kivitengo katika hoteli hiyo ulivyoweza kuvukwa.