KAMATI
ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi
na Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa kazi
nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji
maji  katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza
kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi
inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa wa
Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel
Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati imeona jinsi gani fedha
za serikali zimetumika.

Hata
hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za mkopo  kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila
kitu kinafanywa na makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.
“Inawezekana
kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye component ya
huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.” Alisema Mhe.
Papian.

Aidha
Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani (Wakandarasi)
wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima wawe wameshajua na
kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze kuendesha miradi hii kikamilifu.
Ziara
ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea taarifa
ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya kutembeela baadhi
ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji ya
Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya Makongo na Salasala.
Kamati
pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji
Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu chini na
Ruvu Juu.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema, Mradi wa uboreshaji wa
huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es
Salaam na Pw
ani unaendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es
Salaam na katika Miji ya Bagamoyo na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2
kukamilika.
“Mradi huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na
unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi
Mwang’ingo alitaja kuwa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na
kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi
milioni 6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na
ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.
Kazi nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia
za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa
jumla ya kilomita zipatazo 477.
“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Salasala, Bunju,
Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni,
Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo
wa Ruvu Juu.” Alifafanua.
Aidha maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na
Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na
Msigani na maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu
uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston
T. Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo
hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya ya
Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.
“Tayari tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji
mengi ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni
uhaba wa fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema
Bw.Msongole.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo(kushoto), akifafanua jamnbo mbele ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kulia) na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, walipotembelea ujemnzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji la Salasala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo Januari 20, 2018.
 

 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel; Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
 Kaimu Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, (katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
 Taswira ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
 Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
 Modester Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel
Papian, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya.
 Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.

Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
 Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
 Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
 Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
 Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
  Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.

  NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, RUVU