Watu 20 wameuawa kufuatia mapigano yaliyotokea kati ya makundi ya wanamgambo hasimu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Mapigano hayo yamesababisha kusitishwa kwa safari za ndege, katika uwanja wa kijeshi wa Maitiga, ambao ndio wa pekee wa kimataifa mjini Tripoli.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters ndege zipatazo tano zimeathiriwa na mapigano hayo.
Seikali ya Maridhiano ya kitaifa ya Libya imesema shambulio hilo ni jaribio la kundi moja la wapiganaji kuachiliwa kwa wafuasi wake waliokuwa wakishikiliwa na kundi wanalopingana nalo.
Ghasia za mara kwa mara zimekuwa zikitokea mjini Tripoli tangu mweaka 2011.