Karibu watu 1,500 wamehamishwa kutoka visiwa vya Papua New Guinea, ambapo mlima ambao umekuwa umetulia kwa muda mrefu ulianza kulipuka, kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

Volkano katika kisiwa cha Kodovar ilianza kutoa moshi na majivu wiki iliyopita, na kusababisha kuhamishwa kwa zaidi ya watu 500 kwenda kisiwa kilicho karibu cha Blup Blup.
Baada ya mlipuko kuzidi sasa wale waliokimbilia kisiwa cha Kodovar sasa watahamishiwa kwingine.
Papua New Guinea ni nyumbani kwa milima kadhaa ya volkano.
Walioshuhudia huko Blup Blup kusini mwa kisiwa cha Kadovar waliripoti mlipuko mkubwa kutoka kwa volkano siku ya Ijumaa na moto mkubwa ukitoka kwenye mlima huo.
Wanasayansi baadaye waligundua viwango vikubwa vya gesi ya sulphur dioxide kutoka na volkano hiyo.
Map locator
Image captionZaidi ya 1500 wahamishwa baada volkano kulipuka Papua New Guinea