Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa
ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akiongea na wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Iringa lilofanyika katika ukumbi wa CCM sabasaba na kutoa jumla ya shilingi milioni
kumi na
tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini

 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa
ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa UWT manispaa ya Iringa
 Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa
ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa
ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya
umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni nne
(4,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa Mjini kwa ajili ya kuendeleza
miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.


 


Pesa hizo zimetolewa wakati wa
baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Iringa Mjini mkoani (UWT) lilofanyika
katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo Iringa Mjini na kuhudhuriwa na
wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati na Rose
Tweve





Akizungumza katika baraza hilo MNEC
Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa
wilaya ya Iringa Mjini kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi
wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.





Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema
kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye
vikundi vya uzalishaji kama
vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya
ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza
kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema
Asas 





Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kuanzisha
duka kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo
bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000)
ili wafikie malengo ya kujiendesha na kuacha kuwa tegemezi.





Aidha Asas alimpongeza mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha
wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba  kwa kutoa
kiasi cha shilingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema
kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata hivyo kwa kata zote 18
za wilaya ya Iringa Mjini atachangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000).





Kwa hili sipepesi macho nampongeza
sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata
mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa
kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia
mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya
ya Iringa Mjini Frola Kapalia alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada
mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ambapo ukipiga
mahesabu utagundua kuwa ametoa jumla ya shilingi milioni kumi na
tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini

“Ametoa shilingi mioni nne kwa UWT
na ametoa milioni tisa (9,000,000) kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa
mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kapalia