AMTAKA AMKUBUMKE
Kwenye mahojiano hayo, Rehema alimtaka Diamond kabla hajaoa akumbuke fadhila zake na aeleze umma ukweli wa penzi lao ili kufuta kile alichonacho moyoni kwani alitarajia baada ya kuwa na mafanikio, angemtafuta angalau kula naye bata, lakini hakuwahi kufanya hivyo ingawa alimuahidi mambo mengi mwanzo wa kusaka mafanikio.
“Kwa sababu nimepita kwenye maisha yake na mpaka yeye kufikia mafanikio aliyonayo kabla hajaoa aweke wazi kwani nina mchango mkubwa sana kwake na aliniahidi mambo mengi kwa sababu hata kabla ya penzi letu nilianza kumsaidia ndiyo baadaye tukazama kwenye penzi zito,” alisema Rehema.
AWALIPUA ZARI NA WEMA
Akizidi kutiririka, Rehema aliwalipua wasichana wote waliopita wa Diamond akiwemo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Wema na kuwaambia kuwa wanapokuwa wanagombana au kurushiana maneno yeye anawaangalia tu kwani anajua kuwa kwa alivyokuwa zamani hakuna ambaye angemgombea. “Nawashangaa akina Zari na Wema ambao kwa sasa wanamgombea wakati ameshang’aa, nawaangalia tu na kuwavutia pumzi mpaka mwisho wa shoo, nione shoo itaishaje.
“Wanamgombea ili iweje? Wanamjua alikotoka? Nimejifunza mengi kupitia wanawake wenzangu, Diamond ninamjua mimi vizuri, laiti wangemjua kama ninavyomjua, hata wasingegombana,” alisema Rehema.
AWEKA NUKTA
Rehema alimalizia kwa kusema kuwa, anamsihi Diamond kuwakumbuka watu wote waliopita kwenye maisha yake kwani bila kufanya hivyo hataendelea na atakuwa na maadui wengi ambao mwisho wa siku, wote wanaweza kumkwamisha kwa kumuombea mabaya.
DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa Diamond juzi Jumamosi, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa chatting kwenye WhatsApp hakujibu.
KUMBUKUMBU ZA IJUMAA WIKIENDA
Ijumaa Wikienda lina kumbukumbu adimu za Diamond na mrembo huyo walipokutana miaka ya nyuma, enzi hizo Diamond akiwa angali bado hana umaarufu.
HANA TATIZO NA MTU
Kwenye mahojiano mengi ya hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa ameshamaliza tofauti na warembo wake wote waliowahi kuwa wapenzi wake wakiwemo, Wema, Jokate Mwengelo na Penniel Mngilwa ‘Penny’ lakini hakumtaja Rehema.
Stori: Hamida Hassan, Dar
|
0 Comments