MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kati ya kina baba 226 waliofi ka ofisini kwake kuitikia wito wa kufanya mazungumzo juu ya hatma ya watoto wao waliokuwa wamewatelekeza, 205 wamekubali kwa maandishi kuwa watawajibika kuwatunza.
Jumatatu ya wiki hii, akina mama waliotelekezwa na wazazi wenza walijitokeza kwa wingi ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Ilala Boma kuwasilisha malalamiko yao juu ya wazazi wenza waliowatelekezea watoto. Akizungumzia kuhusu mchakato huo uliokuwa wa siku tano na kutakiwa kumalizika jana, Makonda alisema mafanikio ni makubwa kwa kuwa kwa asilimia kubwa kumekuwa na faida kutokana na hatua hiyo aliyoichukua.
Makonda alisema mbali na wanaume hao 205 kukubali kwa maandishi, wanaume 21 wamekubali kupimwa Vinasaba (DNA) ili kubainisha kama kweli wao ni wazazi wa watoto husika waliofikishwa ofisini kwake. Alisema zaidi ya kinamama 10,000 wamefika kupata huduma na ambao kati yao kinamama 4,000 wamesikilizwa na kubainisha wazi kuwa kila mwanamke aliyefika kwenye ofisi yake anasikilizwa huku mtoto akipatiwa bima ya afya bure.
|
0 Comments