Aliyekuwa mkuu wa FBI nchini Marekani, James Comey ameiambia BBC kuwa haamini kuna kiongozi yoyote wa karibu na Rais wa Marekani Donald Trump anaweza kumbadilisha tabia yake.
Anasema tabia zake zinahatarisha hadhi ya nchi.

Kabla ya kufukza na Trump Comey aliongoza uchunguzi dhidi ya kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.
Akizungumza katika kipindi cha Newsnight Comey anasema tabia za Trump zinaathiri wale wanaomzunguka.
"Nadhani tabia yake inaathiri hasa hasa kwenye suala la ukweli na jambo la msingi ni jinsi tabia hizo zinavyoathiri taasisi na watu wa karibu wake.Ana tabia a kuongea uongo na kuwa lazimisha wale wanamuunga mkono kukubalina naye na kuamini"
Trump alimshutumu Comey kuwa anayoyazungumza na uongo na siasa zake za ubaguzi.

Je tumefikaje hapa?

Hadithi hii inaanzia wakati wa uchaguzi wa urais mnamo 2016, wakati Bwana Comey alikuwa mkurugenzi wa FBI director, na uchunguzi kuhusu namna mgombea wa urais wa chama cha Democrat Hillary Clinton alivyozishughulikia barua pepe za siri katika kompyuta binafsi wakati akiwa waziri wa mambo ya nje.
Barack Obama wakati w akuapishwa kwa Comey katika FBI mnamo 2013Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarack Obama wakati w akuapishwa kwa Comey katika FBI mnamo 2013
Mnamo Julai 2016, Comey alisema kwamba hakuwa na umakini katika namna alivyozishughulikia barua pepe hizo, lakini FBI haitomshtaki.
Hatahivyo mnamo Oktoba, sikukadhaa kabla ya uchaguzi, alituma barua bungeni akiliarifu kwamba FBI linaanzisha upya uchunguzi baada ya kugundua barua pepe zaidi.
Barua hiyo ilifichuliwa kwa umma - na Hillary Clinton akasema hatua hiyo ndiyo iliompa Trump ushindi.
Mnamo November, FBI lilisema limekamilisha ukaguzi wa barua pepe hizo mpya zilizogunduliwa na kwa mara nyingine likasema halitomshtaki.
Na bwana Trump alipopata urais, Bwana Comey alisema kuwa alijaribu kumshurutisha aape kumtii - Jambo ambalo rais analikana pakubwa.
Ushahidi wa Comey ulitazamwa na mamilioni ya watu MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUshahidi aliotoa Comey bungeni ulitazamwa na mamilioni ya watu Marekani
Mnamo Machi 2017, wakati uchunguzi ulipokuwa unafanywa na FBI kuhusu tuhuma za ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi inatuhumiwa kwamba Trump alimshinikiza Comey kutangaza wazi kwamba rais hatochunguzwa kibinafsi - jambo ambalo mkurugenzi huyo wa zamani wa FBI alikataa kufanya hivyo.
Baadhi ya wanasiasa wa Democrats walimlaumu Comey kwa kumfanya Bi Clinton apoteze kura katika uchaguzi , huku wafuasi wa Trump walihisi kwamba anamlenga rais katika uchunguzi huo.
Alifutwa kazi na rais Trump mwezi Mei, na alipata taarifa kuhusu kutimuliwa kwake katika vyombo vya habari nchini.
Comey alihojiwa bungeni kuhusu uchunguzi huo wa uwezekano kuwepo uhusiano kati ya kampeni ya Trump na Urusi na kutimuliwa kwake, na alimthumu rais kwa kusema urongo na kumchafulia jina.

Orodha ya maafisa wa serikali ya Marekani waliofutwa kazi na rais Donald Traump tangu achukue mamlaka.

  1. Rex Tillerson, waziri wa maswala ya kigeni - 13 Machi 2018
  2. Gary Cohn, Afisa mkuu wa masuala ya kiuchumi - 6 Machi 2018
  3. Hope Hicks, Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Whitehouse - 28 Februari 2018
  4. Rob Porter, Katibu katika Ikuku ya White House- 8 Februari 2018
  5. Andrew McCabe, Naibu mkurugenzi shirika la FBI - 29 Januari 2018
  6. Tom Price, Waziri wa afya - 29 Septemba 2017
  7. Steve Bannon, Afisa mkuu wa mipango - 18 Agosti 2017
  8. Anthony Scaramucci, Mkurugenzi wa mawasiliano - 31 Julai 2017
  9. Reince Priebus, Afisa mkuu wa wafanyikazi wa umma - 28 Julai 2017
  10. Sean Spicer, Waziri wa habari - 21 Julai 2017
  11. James Comey, Mkurugenzi wa shirika la FBI - 9 Mei 2017
  12. Michael Flynn, Mshauri wa maswala ya usalama - 14 Februari 2017
  13. Sally Yates, Kaimu Mwanasheria Mkuu - 31 Januari 2017
  14. Preet Bharara, Mwendesha Mashtaka wa New York federal prosecutor - 11 Machi 2017
  15. Paul Manafort, Meneja wa Kampeni wa Trump - 19 Agosti 2016