Serikali imesema haitawarudisha shuleni kupitia mfumo rasmi wa elimu wanafunzi waliopata ujauzito kwa namna yoyote kufanya hivyo ni kuhalalisha ngono, kinyume na taratibu za nchi na utamaduni.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati bungeni Dodoma leo, baada ya kuulizwa mpango wa serikali juu ya waliokatishwa masomo kwa sababu za kupata ujauzito hususani kwa kubakwa.
“Serikali haina mpango wa kuwarudisha shule wanafunzi waliopata uajauzito kwa mfumo rasmi bali imeandaa fursa nyingine za elimu kama kuwapa elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya elimu ya watu wazima ili waweze kujikwamua kimaisha,”.
Katika hatua nyingine Ole Nasha amesema kuwa, katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi nchini, serikali imeongeza udahili wa walimu wa masomo ya sayansi katika vyuo ambavyo vilikuwa havitoa kozi hizo, ikiwemo chuo cha Chuo cha Kilimo (SUA) na Mzumbe pamoja na kuongeza vifaa vya kufundishia masomo ya sayansi.
0 Comments