Raisi wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hakuna uwazi endapo mkutano pamoja na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un utafanyika kama walivyokubaliana awali, ingawa bado ana matumaini .

Rais Trump ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari na ndipo walipomuuliza endapo mkutano baina yao utafanikiwa na Raisi kujibu kuwa wanapaswa kuwa na subra na kusubiri matokeo.
Pamoja na majibu hayo ya raisi wa Marekani, Pyongyang imetishia kusitisha mazungumzo hayo endapo Mamlaka mjini Washington itaendelea kushinikiza juu ya uwepo silaha za nyuklia moja kwa moja.
Mamlaka zinaarifu kuwa matamshi ya Mshauri wa Usalama wa Taifa la Marekani , John Bolton, yamezua hasira juu ya uzoefu wake katika silaha za Libya, ambayo wanaona kama mfano wa mabadiliko ya utawala.
Hasa ni nini kitakachojadiliwa bado haijajulikani lakini Korea ya Kaskazini imealika vyombo vya habari vya kigeni kushuhudia kuteketezwa kwa kinu chake cha nyuklia baadaye mwezi huu.
Taarifa ya Korea Kaskazini,kwa vyombo vya habari vya serikali, inaarifu kuwa nchi hiyo ilikuwa na matarajio makubwa kutokana na mkutano huo, lakini imekatishwa "tamaa kabisa" na maelekezo ya hivi karibuni yaliyotolewa na Marekani.