WATUHUMIWA sita wa kumiliki Blogs, Televisheni na Radio za Mitandaoni bila vibali vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwemo watangazazji wawili wa Clouds Media, Soudy Brown na Shaffih Dauda leo wamefikishwa  katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yanayowakabili.


Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kusomewa shitaka hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Johanes Kalungula amesema kuwa mtu yoyote hawezi kumiliki Radio, Televisheni na mitandao mingine bila kujulikana na endapo itajulikana atashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ya nchi.

Mwanzoni wa mwaka huu serikali iliwataka wamiliki wa mitandao ya kijamii ya ‘blogs’, tovuti na aina nyingine ya vyombo vya habari vya habari vinavyochapisha kwenye mtandao kujisajili chini ya TCRA na kupewa leseni zitakazowawezesha kufanya kazi hizo kwa kufuata misingi ya sheria za nchi.

VIDEO: MSIKIE HAPA KALUNGULA KIFUNGUKA