Kevin York Systrom
WAANZILISHI wa mtandao wa Instagram wametangaza wiki chache zijazo watajiondoa kabisa kujishughulisha na kampuni hiyo na kubaki kama watumiaji wengine wa kawaida.


Image result for Mike Krieger
Kevin York Systrom na Mike Krieger

Kevin York Systrom ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu na Mike Krieger, Mkuu wa Ufundi wametangaza uamuzi huo ikiwa ni miaka sita baada ya kuiuza kwa wamiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg,  na kwamba watabakia kama watumiaji wengine wa kawaida.
Katika taarifa yao ya pamoja wamesema wanajipanga kufanya udadisi upya katika masuala ya Mitandao ya Kijamii. Wamesema walipoanza mtandao huo wa Instagram umekua kutoka watumiaji 13 mpaka mamilioni ya watumiaji duniani kote kwa sasa.