Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji


Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future

 JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future

NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.

JAMII
ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada
ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki
mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa
katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.

Wakizungumza
wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali
walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa
zinamilikiwa na wanaume.

“Kwenye
kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na
kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha
maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi

Wanawake
hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi
kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya
mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila
la wabarbaigi.

Tunaishukuru
serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi
kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila
elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.

Naye
mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana
kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na
kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.

“Sisi
kabila letu ni watu wa kuhama hama hivyo baada ya kupata hati miliki za kimira
sasa hatuwezi kuhama tena kwa kuwa tunamiki ardhi kisheria zinazotuwezesha
kuboresha makazi yetu na kutufanya tuishi na kufanya shughuli zetu sehemu moja”
alisema Ntasham

Ntasham
alisema Mradi wa LTA wa feed the future unaofadhiwa na USD umetoa elimu kwa
kabila la barbaigi na kusaidia kuanza kuondokana kwa kiasi chake mfumo dume kwa
kuwawezesha wanaume wa kabila hilo kuwagawaia wanawake ardhi na kuzikatia hati
miliki za kimila.

“Saizi
umeona wanawake na wanaume wanafuraha kwa pamoja kwa kuwa kila mmoja anamiliki
ardhi yake ambayo inamuwezesha kufanya jambo analolitaka kwa wakati wake
tofauti kama ilivyokuwa hapo zamani” alisema Ntasham

Akizungumza
na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo diwani wa kata ya Idodi Onesmo
Mtatifikolo alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya
matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi
ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

Mtatifikolo aliongezea
kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa
miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika
taasisi za kifedha zikiwemo benki.

“Usajili
wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha
uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mtatifikolo

Aidha
Mtatifikolo aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize
kupima vijiji vyote vya kata hiyo  huku akivikumbusha vijiji vyote
vya kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza
maendeleo ya nchi. 

“Tunataka
katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya
mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani
(USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili
kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Mtatifikolo.

Mtatifikolo
aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu
mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao
bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi
hilo.

Awali naibu
mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa aliwapongeza wataalamu
wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Kitisi kupima
maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye
maendeleo ya kiuchumi.

“Baadhi
ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa
wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za
kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa
kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao”
alisema Msigwa