Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb)
akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Mara baada ya kuwasili Mkoani
Simiyu kwa ziara ya kikazi ya siku moja, leo Alhamisi Octoba 2018. (Picha Zote
Na Mathias Canal,WK)

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.





Na mathias Canal-WK, Bariadi-Simiyu

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba  (Mb) leo
Alhamisi Octoba 2018 amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya
kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika
katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani
Simiyu.

Katika
maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo
ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya
teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata
nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

"Nitoe
wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na
Shinyanga wajitokeza  kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa
muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt
Tizeba

Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa
kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu
waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi
wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani
wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya
kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko
ya bidhaa zao.

Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu
isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa
rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa
(Mb) siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya
Jumapili Oktoba 28, 2018.

MWISHO