Klabu ya Real Madrid imemfuta kazi kocha wake Julen Lopetegui baada ya miezi minne na nusu ya kudumu klabuni hapo.
Mhispania huyo alichukua mikoba kutoka kwa Zidedine Zidane mwezi wa sita ambapo kupoteza kwenye mchezo wa El Clasico dhidi ya Barcelona ulikuwa mchezo wa tano kufungwa katika michezo sita waliyocheza ya hivi karibuni.

Huu ni mwanzo mbaya zaidi wa Real Madrid tangu walipofanya hivyo mwaka 2001-2002.
Madrid ambayo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara tatu,ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa La Liga.
Mikoba ya Lopetegui, 52 sasa itarithiwa na kocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Santiago Solari ambaye amewai kuwa mchezaji bora Madrid na kutengeneza ufalme wake.
Santiago Solari aling'ara miaka ya nyuma akiwa mchezaji wa Madrid
Image captionSantiago Solari aling'ara miaka ya nyuma akiwa mchezaji wa Madrid
Lopetegui alishiriki mazoezi na wachezaji siku ya Jumatatu ingawa matarajio yake yamefutwa na kikao cha dharura cha bodi ya timu hiyo kilichokaa siku ya Jumatatu jioni.
Taarifa ya klabu inasema kwamba 'Kumekuwa na utofauti mkubwa sana kati ya uwezo wa viongozi wetu (Real Madrid) na matokeo tunayoyapata mpaka sasa'.
Wachezaji wanane wa Madrid ni sehemu ya majina 30 yaliyotajwa kuwania Ballon d'Or ya mwaka 2018.
Kocha mteule Solari atakumbana na ratiba rahisi ukiitazama ambapo ataanzia kwenye mchezo wa kombe la ligi ya Hispania dhidi ya timu ya daraja la nne Mellila, siku ya Jumatano.
Real itakutana Valladolid katika mchezo wa sita wa La Liga siku ya Jumamosi ambapo Novemba 7 itaikaribiana na Viktoria Plzen kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya, ikifuatia mechi dhidi ya Celta Vigo.
Hii inakuwa mara ya pili kwa kocha Lopetegui kufukuzwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kuondoshwa kwenye kikosi kilichotakiwa kusafiri kuelekea Urusi kwenye Kombe la Dunia siku mbili baada ya kugundulika amesaini mkataba wa Real Madrid.
Chama cha Soka Hispania kiliamua kumfukuza baada ya kuwekwa wazi kuwa yupo katika mazungumzo ya mwisho kupata kibarua cha kuinoa Real Madrid baada ya mashindano ya Kombe la Dunia kumalizika.
Real Madrid ina alama 14 kati ya 30 katika ligi mpaka hivi sasa, imepata alama moja katika michezo mitano iliyopita, matokeo mbaya Zaidi tangu mwaka 2008-2009 ilipocheza michezo mitano bila kupata hata pointi moja ilipokuwa chini ya Juande Ramos.
Madrid haijawa na matokeo mazuri baada ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo
Image captionMadrid haijawa na matokeo mazuri baada ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo
Madrid ipo alama sita juu ya timu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja na alama saba nyuma ya vinara Fc Barcelona.
Imepoteza michezo mine na sare moja kwenye michezo mitano.
Alama saba nyuma ya vinara kwenye La Liga Barcelona baada ya mchezo wa El Clasco, ambapo haina utofauti wa goli.
Ilipoteza dhidi ya CSKA Moscow kwenye Klabu Bingwa Ulaya na kupata ushindi mwembamba dhidi ya Viktoria Plzen
Kuondoka kwa Julien Lopetegui kunafungua milango kwa aliyekuwa kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ambaye anapewa kipaumbele kuteulewa kuwa kocha mpya wa Real Madrid kwani hana kazi tangu atimuliwe Chelsea mwezi wa saba.
Lakini vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamechelewa, kwa wakati huu Solari, 42, anachukua nafasi iliyoachwa wazi ambapo anaweza kuwa kioo cha Zidane kwani nae anatokea timu B lakini Solari ni maarufu kama Zidane.
Zidane alichukua nafasi ya Rafael Benitez ambaye alifukuzwa mwezi Januari 2016 na Mfaransa huyo alikabidhiwa timu kama mwangalizi kwa muda kabla ya kufanya maajabu ya kuwa Kocha mwenye mafanikio makubwa akiwa ametwaa makombe matatu ya Klabu Bingwa Ulaya, kabla ya kujiengua mwezi wa tano mwaka huu.
Kiungo wa zamani wa Real na Argentina Solari alimrithi Zidane katika ukocha wa timu ya vijana ambayo ipo katika ligi daraja la pili ikiwa nafasi ya tano alama tatu nyuma ya vinara Ponferradina.
Kwa mjibu wa sheria ya Hispania, Kocha wa muda anatakiwa kukaa wiki mbili lakini anahitajika kuteuliwa rasmi baada ya siku 15.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ambaye alishinda La Liga na Copa del Rey katika miaka mitatu akiwa Santiago Bernabeu kuanzia mwaka 2010-13, pamoja na kocha wa zamani wa Everton Roberto Martinez ambaye aliifikisha Ubeligiji nusu fainali ya Kombe la Dunia wamekuwa wakihusishwa na kupewa fursa ya kuwa kocha wa Real Madrid.