KUTOKUWEPO kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, katika msimu huu wa tamasha la muziki la Tigo Fiesta, kumeelezewa na mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G. Habash, kuwa ni pengo kubwa.
Kwa muda wa miezi kadhaa Ruge amekuwa akipata matibabu kutokana na matatizo ya figo na sasa yuko nchini Afrika Kusini.  Clouds Media Group ndiyo wanaoendesha tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo.


Akipiga stori na Chanzo cha habari hiiGadner amesema msaada wa Ruge siyo tu kwenye Fiesta, bali kwenye kampuni nzima na taifa kwa ujumla, hivyo kukosekana kwake lazima kuwepo na pengo kwa namna moja ama nyingine.

Aidha, amesema bosi wao huyo amewafundisha vitu vingi hivyo wanajitahidi kufanya kila mbinu kuhakikisha tamasha hilo linakuwa la ubunifu wa hali ya juu tofauti na miaka mingine iliyopita.

Baada ya kuzunguka kwenye mikoa kadhaa hapa nchini, hatimaye Tigo Fiesta inatarajiwa kufanyika Jumamosi hii, Novemba 24, 2018, katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

MSIKIE GARDNER AKIFUNGUKA HAPA