MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,wakati akitangaza kamati ya watu 17 na kuwapa majukumu ua kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa na amani, maadili na utamaduni wa mtanzania unadumishwa

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao leo ofisini kwake jijini Dar kuhusu kukomesha Ushoga Dar


*Awataka wakazi wa Dar es salaam wenye picha za ngono kwenye simu zao kuzifuta kabla ya jumatatu.


MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu 17 na kuwapa majukumu ua kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa na amani, maadili na utamaduni wa mtanzania unadumishwa.




Akizungumza na wanahabari leo jijini, Makonda amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuhakikisha na kuwatambua mashoga wanaojitangaza na wasiojitangaza katika mitandao ya kijamii wanajulikana ikiwemo facebook, whatsaap na Instagram.




Aidha kamati hiyo itakuwa jukumu la kuwatambua wanaojitangaza na kufanya biashara ya ngono katika mitandao ya kijamii na wale wanaofanya utapeli hasa wa kutumia mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya watu maarufu.




Makonda amesema kuwa kamati hiyo itahusisha bodi ya filamu, Mamlaka ya mawasiliano (TCRA,) polisi na madaktari na kituo cha huduma hiyo itakuwa Mburahati na amesema kuwa kwa yeyote atakayegundulika kujihusisha na vitendo hivyo atatangazwa na kutaja anayeshiriki naye na kuchukuliwa hatua za kisheria.




Aidha amesema kuwa kabla ya jumatatu wana Dar es salaam walioweka picha za ngono kwenye simu zao wajitahidi kuzifuta kwani TCRA wana uwezo mkubwa.Mwisho ametoa rai kwa kwa wakazi wote wa Dar es salaam kushikamana dhidi ya mapambano hayo ili kulinda maadili yetu.