Mkuu wa Wilaya Newala Mhe Aziza Mangozongo akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Kuhakiki Majina ya Wakulima katika Makonga Amcos na kubaini Watu wawili(2),Karani wa Chama cha Msingi Makonga Asma Rajabu kwa kosa la  kumuandikia malipo Hewa  ya kilo Hewa 221kg ya korosho na Mohamed Hamisi Namkunga ambaye ameandikisha Majina Hewa tofauti Mara Tatu na Account Hewa kwa lengo ya kufanya Malipo Hewa.Mh.Aziza amesema huo ni mtindo mpya wa Kangomba. 

Mkuu Wa Wilaya Newala amethibitisha kukamatwa kwa watu hao leo  na kusema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili Sheria ichukue mkondo wake.

Aidha  amewataka Viongozi wa Vyama vya Msingi/Amcos na Makarani kuwa Wazalendo na kuandika Malipo sahihi kwa Wakulima.

Newala tutahakikisha kwa Kila hatua tunakuwa makini mpaka Mwisho. 


Imetolewa 

Mwansishi Wetu

Newala.