Wachezaji watano waliyoteuliwa kuwania tuzo ya BBC ya Mchezaji wa bora wa kandanda barani Afrika mwaka 2018 wametangazwa.
Wachezaji waliyoorodheshwa mwaka huu ni Medhi Benatia (Morocco), Kalidou Koulibaly (Senegal), Sadio Mane (Senegal), Thomas Partey (Ghana) na Mohamed Salah (Misri).

Upigaji kura umeanza rasmi Novemba 17(Leo Jumamosi) saa Nne usiku kwa saa ya Afrika Mashariki na utakamilika mwezi Desemba 2 saa Tano usiku.
Mshindi wa tuzo hii atatangazwa katika kipindi cha BBC World News Disemba 14 saa mbili unusu kwa saa ya Afrika Mashariki.
Orodha ya waliyoteuliwa imeandaliwa na jopo la wataalamu wa kandanda barani Afrika.
Mshambuliaji wa Liverpool Salah ndiye aliyeshinda tuzo ya mwaka jana.
Wachezaji wengine waliyoshinda tuzo hiyo ni pamoja na Jay-Jay Okocha, Michael Essien, Didier Drogba, Yaya Toure na Riyad Mahrez.

Watakaowania tuzo ya mwaka huu:

Beki wa kati wa Juventus Benatia, 31, ameshinda ligi mara nne mfululizo mwaka huu - Mbili kati hizo akiwa na Bayern Munich na mbili zingine akiwa Juve.
Pia alikuwa nahodha wa Morocco katika michuano ya Kombe la Dunia ya msimu wa joto mwaka huu.
Mlinzi wa Napoli Koulibaly, 27, aliiwakilisha katika klabu kuchuana dhidi Juve katika kinyang'anyiro cha fainali ya ligi ya Serie A ya Italia ikiwa ni pamoja na ushindi maarufu dhidi ya miamba hao wa ligi ya mabingwa.
Aliichezea Senegal dakika zote 270 katika michuano ya Kombe la Dunia.
Mshambuliaji wa Liverpool Mane, 26, pia aliichezea Senegal katika michuano ya Kombe la Dunia, ambapo aliiongoza taifa kushinda Japan.
Alikuwa mfungaji bora wa pili katika ligi ya mabingwa wa Ulaya msimu uliyopita-aliifungia Liverpool mabao 10, ikiwa ni pamoja na bao moja aliyoifunga walipochapwa 3-1 na Real Madrid katika fainali.
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Partey, 25,alichaguliwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Diego Simeone baada ya kuonyesha umahiri ikiwa ni pamoja na kuwa mchezaji wa ziada katika fainali ya ligi ambapo waliishinda Marseille.
Aliifungia Ghana katika mechi ya kimataifa ya kirafiki walipochuana na Japan na Iceland.
Mshambualiaji wa Liverpool Salah, 26, alishinda taji la mfungaji wa mabao mengi zaidi (32) katika ligi kuu ya England mwezi Mei.Sawa na Mane, alifunga mabao 10 katika ligi ya mabingwa kuelekea fainali. Aliifungia Misri mabao yote ya kombe la Dunia.