mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.
Wanajeshi wa kifalme na jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha walishiriki katika maandamano makubwa ya kusherehekea maisha yake yaliyofanyika kabla ya mazishi yake huko Bangkok,

Wachezaji wa Leicester City wanatarajiwa kusafiri nchini Thailand kwa mazishi baada ya mechi yao dhidi ya Cardiff.
Bilionea Vichai alifariki pamoja na wafanyikazi wake wawili, rubani wa ndege aliyokua akisafiria na abiria mmoja baada ya ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.
Walioshuhudia wanasema ndege hiyo ilikuwa tu imemaliza kuondoka uwanjani pale ilipoanza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.
Jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishi
Jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishi
Majeshi ya kifalme wakishiriki katika maandamano ya mazishi ya bwana VichaiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMajeshi ya kifalme wakishiriki katika maandamano ya mazishi ya bwana Vichai
Mazishi yake yataanza na kafara ya kuoga ya waumini wa kibudha ambayo yatafuatiwa na sherehe ya siku saba ya kidini.
Mwandishi wa BBC Jonathan Head, mashariki mwa Asia ambaye anafuatilia sherehe hizo anasema kuwa zinafanywa faraghani,
Ndugu na jamaa zake wanatarajiwa kuwasili wwakati wowote kuazia sasa.
Waombolezaji wanaonekana kupitia milango ya vioo katika mazishi ya bwana VichaiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaombolezaji wanaonekana kupitia milango ya vioo katika mazishi ya bwana Vichai
Watu wa tabaka mbali mbali washiriki shughuli hiyoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu wa tabaka mbali mbali washiriki shughuli hiyo ya kupekee
Suala la hadhi ya mazishi ni muhimu sana nchini Thailand.
"Wakati wa mazishi haya utaona jinsi vito maalumu vitavyotolewa na mfalme Vajiralongkorn -
Pia amesema ''Watu watafuatilia kwa makini sana hii inaashiria jinsi Vichai alivyokua mashuhuri was.
"Alikua mwanabiasha maarufu, lakini zingine zilikumbwa na utata."
Msafara wa mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha mjini BankokHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMsafara wa mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha mjini Bankok
Vichai SrivaddhanaprabhaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionVichai Srivaddhanaprabha aliinunua klabu ya Leicester City mwaka 2010
Mwili wa bwana Vichai uliwasili Thailand siku ya Ijumaa kabla ya mazishi yake .
Nusara Suknamai, Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na mpenzi wake, Izabela Roza Lechowicz, pia walifariki katika ajali hiyo ya ndege ya Jumamosi iliyopita.
Mabaki ya ndege hiyo iliondolewa nje ya uwanja siku ya Ijumaaa.
Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea.
Naibu waziri mkuu Prawit Wongsuwan akimwagia maji bustani la maua la Vichai SrivaddhanaprabhaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNaibu waziri mkuu Prawit Wongsuwan akimwagia maji bustani la maua la Vichai Srivaddhanaprabha
Naibu wa waziri mkuu wa Thailand Prawit Wongsuwan,meneja wa timu ya soka ya wanawake ya Thailand na rais wa shirikisho la kandanda la Thailand ni miongoni mwa wageni wanaohudhuria mazishi hayo.
Kwa picha mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.