![Aaron Ramsey(kulia) alijiunga na Arsenal mwaka 2008](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/159E8/production/_104125588_95d19ca6-689f-4d92-a5ef-44d1f0c8c6d3.jpg)
Chelsea huenda ikabadili msimamo kuhusu mpango wake wa kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 27,kutokana na kuimarika kwa mchezo wa Ross Barkley, 24, na Ruben Loftus-Cheek, 22. (Star)
Huku hayo yakijiri, Liverpool imefutilia mbali uwezekano wa kiungo huyo wa kimaatifa wa Wales ambaye yuko tayari kuondoka Gunners bila malipo msimu wa joto kujiunga nayo. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Mhispania Cesc Fabregas, 31, atalazimika kusubiri hadi mwaka mpya kabla ya kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na Cheasea . (Evening Standard)
- Wasiwasi kuhusu De Bruyne Man City
- Arsenal wapewa mtihani wa Spurs Kombe la Carabao
- Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 01.11. 2018
![Suarez amefunga mabao tisa dhidi ya Real Madrid](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/180F8/production/_104125589_e6add3ab-f97d-440b-a1be-f46e9f56ffee.jpg)
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick katika mechi ya El Clasico. (Sport 890, via Sun)
Liverpool inajiandaa kumpatia kandarasi mpya mlinzi wa England defender Joe Gomez, 21, miaka tatu na nusu hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Brazil Fabinho huenda akaondoka Liverpool miezi sita tu baada ya kuhamia Anfield kwasababu ''ameboeka''. (Le Parisien - in French)
Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema "Hatutapoteza muda wetu kujadili hilo" alipoulizwa kuhusu tetesi za Real Madrid kutaka kumpatia kazi kama meneja wake mpya. (AS, via VTM Nieuws)
![Wigan manager Roberto Martinez](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/2550/production/_104125590_martinez.png)
Tottenham inapania kumnunua kiungo wa kati wa Watford, mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25. (Mirror)
Meneja wa Manchester United boss Jose Mourinho ana mpango wa kufanya usajili zaidi ya moja wakatu dirisha la uhamisho litakapo funguliwa mwezi Januari- Ni mara ya kwanza klabu hiyo itafanya hivyo katika kipindi cha miaka 10. (Manchester Evening News).
Borussia Dortmund inataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Brahim Diaz, 19. (Metro)
Lakini meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo "itafanya kila iwezalo" kumshawishi asiondoke. (Manchester Evening News)
![Dele Alli kusalia Spurs hadi 2024 baada ya kutia saini mkataba mpya](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/4C60/production/_104125591_cb2b1e6a-0c50-45b4-8601-84144ebd004e.jpg)
Kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 22, anasema "kushinda kombe sio kila kitu ukizingatia umri wangu" baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka sita na Spurs mapema wiki hii. (Telegraph)
Wanaotunga sheria za kandanda huenda wakajadili mabadiliko yatakayo fafanua sheria ya kugusa mprira kwa mkono na kuondoa "makusudi". (Telegraph)
Wachezaji wa Fulham watalazimika kukubali kupunguziwa mshahara endapo wataondolewa wakatika ligi ya Primia. (Mail)
Bora kutoka Alhamisi
![Raheem Sterling](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/4684/production/_104125081_3545b0e8-4e02-4e99-a174-826e362986ec.jpg)
Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye kandarasi yake inamalizika mwisho wa msimu huu, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya.
Hatua hiyo huenda ikatia kikomo shinikizo za mashabiki kutaka kiungo huyo kuondoka klabu hiyo kutokana na utenda kazi wake duni uwanjanani. (Manchester Evening News)
Aaron Ramsey, 27, kiungo wa kati wa Wales, ameambiwa na Arsenal anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Mail)
![Antonio Conte aliongoza Chelsea kushinda kombe la FA mwezi Mei](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/94A4/production/_104125083_2fc9087f-34e9-4990-89ec-f9b47b9e70c3.jpg)
Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte bado anapigiwa upatu kuchukua wadhifa wa kuwa mkufunzi mkuu katika klabu ya Real Madrid licha ya tetesi za mapema wiki hii kwamba hakuna uwezekano huo. (AS)
Juventus inatarajiwa kumwinda kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Uhispania Juan Mata, 30 mwezi Januari.
Mata anahudumia mkondo wa mwisho wa kandarasi yake katika uga wa Old Trafford. (Evening Standard)
0 Comments