Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  Mafanikio yaliyopatikana katika Wilaya hiyo kwa kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya  awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli


Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae

Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Newala linavyoonekana kwa nje

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii,Newala ,Mtwara.



Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Newala, Mussa Chimae amesema tangu kutangazwa kwa
operesheni korosho ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Newala wamezunguka  Wilaya nzima kutoa elimu kuhusu nini
kifanyike kupitia agizo la Rais Magufuli kuwa Serikali itanunua Korosho
yote nchini.





Akizungumza
na Waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Wilayani Newala Chimae
amesema kuwa  wamezunguka kwa wananchi kutoa elimu juu ya namna zoezi
hilo litakavyoendesha ikiwa ni pamoja na kuwataka watendaji wa vijiji na
kata kusimamia zoezi hilo kwa makini hili kusitokee malalamiko yoyote.




"Sambamba
na zoezi la uhakiki wa taarifa za wakulima pia tumetoa maagizo kwa
watendaji wa mitaa na kata kusimamia zoezi la uingizaji wa korosho
kwenye maghala na kuhakikisha kuwa hakuna korosho inayoingia kutoka nje
ya mitaa au kata zao ili kudhibiti korosho za magendo zinazoingizwa
kutoka nchi jirani," alisema Chimae.





amesema
kuwa Halmashauri ya Newala ni moja ya Halmashauri zinazopakana na nchi
jirani ya Msumbiji ambapo kwa upande wa majirani zetu kwa sehemu nao
wanalima zao la Korosho hivyo wamejipanga kwa kila namna kwa
kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Kuwa hakuna korosho
kutoka nchi jirani itakayopenya nchini kupitia milango ya Wilaya hiyo.





amesema
kuwa tayari askari wa JWTZ Wamejipanga katika Maghala na wameimarisha
ulinzi kwa kukagua na kulinda korosho hili isije mtu akatokea akatia doa
wilaya yake kwa kufanya vitu tofauti na maagizo ya Rais.