MARCUS Rashford hakuwahi kupewa penalti kupiga ndani ya Manchester United lakini ile ambayo aliipiga usiku wa kuamkia jana imesababisha jina lake liwe gumzo kutokana na kuwa ilikuwa ni ya ushindi muhimu kwa timu yake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Straika huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 21, aliamua kubeba jukumu la kupiga mkwanja huo dakika ya 90 ambao umesababisha United ifuzu kucheza robo fainali, huku kipa mkongwe wa PSG, Gianluigi Buffon akibaki akiwa hana la kufanya.

Penalti hiyo ilikuwa gumzo kutokana na mazingira, muda, umuhimu huku nyuma yake
kukiwa na straika mwenzake, Romelu Lukaku ambaye tayari alikuwa ameshafunga mabao mawili katika mchezo huo ambao United ilishinda mabao 3-1. Ushindi huo umewashangaza wengi kwa kuwa haikutegemewa kwa timu hiyo kupindua matokeo na kusonga mbele kwa kuwa katika mchezo wa kwanza walifungwa mabao 2-0 wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Wachezaji wengi wa United ambao hawakuambatana na timu hiyo Ufaransa kutokana na kuwa majeruhi, walirekodi video wakiwa nyumbani kwao wakirukaruka kwa furaha huku wakiipongeza timu na kumpongeza ‘dogo’ kwa kuchukua maamuzi magumu.

RIO FERDINAND: NAMKUBALI SANA RASHFORD
Akizungumzia kilichotokea, beki wa zamani wa United, Rio Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, alisema kuna tofauti kubwa kati ya mchezaji mzuri na mchezaji wa kiwango cha juu. “Namkubali na ninampenda Rashford, alichofanya ni kuufuata mpira na kuuomba, nilichopenda kwake ni kuwa alijiamini na akaona hakuna ambaye anaufuata mpira baada ya mwamuzi kusema kuwa ni penalti.

“Naamini alichokiwaza muda anaenda kupiga penalti alisema ‘huyu ndiye mimi na huu ndiyo muda
wangu’, hiyo ndiyo tofauti ya mchezaji mzuri na mchezaji wa kiwango cha juu, huyu kijana ni mchezaji wa kiwango cha juu,” alisema.
UKAKU AFUN-GUKA
Akizungumzia uamuzi wa Rashford kupiga penalti hiyo, Lukaku alisema: “Nina furaha kwa kuwa amefunga, alinifuata na kuniambia anahitaji kupiga, nikamwambia ‘huu ni muda wako, fanya hivi kwa ajili yako na kwa faida yetu’