Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi.
- Marekani yaishuku Urusi kutengeneza silaha za nyukilia
- Mwili wa Etienne Tshisekedi kuwasili DR Congo leo kwa mazishi
- K-Lynn asema anamkumbuka sana mumewe Mengi
Vazi alilovalia ni maarufu nchini kwa wanaume wa Fiji likifahamika kama na jina Suti ya Sulu.
Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji.
Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra.
Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino.
Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kukutumia pini.
Baadhi ya Wakenya walitoa maoni haya kwenye ukurasa wa Twitter:
Sulu zilivaliwa na watu wa Fiji Tangu enzi za ukoloni katika katika karne ya kumi na tisa. Mwanzo zililetwa na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga na katika kipindi hiki sketi hizi zilikuwa zikivaliwa na Wafiji kuonyesha kuwa wamejiunga na ukristo.
Sulu za wanawake zinazovaliwa kila siku hufahamika kama sulu-i-ra, na Sulu ndefu wanazovaa rasmi au wakati wa matukio ya sherehe hufahamika kama sulu jaba.
Sulu za wanaume wanazovaa rasmi huitwa -sulu vakataga.
Sulu zilizoshonwa na mifuko huvaliwa kawaida kama vazi la ofisi na rasmi pamoja na shati na viatu vya wazi (sandozi) na upande wa juu huvaa koti na tai.
Katika hali fulani, mtu anapoingia na Sulu kanisani huonekana kama mtu mwenye heshima nchini Fiji.
Sulu zilizoshonwa pia huvaliwa kama sare za polisi na jeshi.
Vazi rasmi la sulu huwana na urefu wa hadi chini ya magoti na hukatwa kwa mathalani umbo la pembe tatu.
Huku uvaaji wa Sulu mara nyingi huwa ni wa lazima kwa Wafiji wakati fulani, baadhi ya jamii wakati mwingine hukatazwa kuzivaa.
0 Comments