Mshambuliaji wa Aston Villa Jonathan Kodjia amefunga goli pekee liloamua mchezo wa baina ya Ivory Coast na Afrika Kusini.
Mchezaji huyo aliunganisha pasi safi kutoka kwa Max Gradel kwa kupiga shuti fupi lilomshinda kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams katika dakika ya 64.

Mshambuliaji mwengine hatari wa Ivory Coast, Nicolas Pepe 23, aligongesha mwamba kipindi cha kwanza, na shuti lake la mkwaju wa faulo kuokolew na Williams kipindi cha pili.
Huu ni mchezo wa pili wa kundi D, jana Jumapili Morocco iliifunga Namibia 1-0.
Ivory Coast - ambayo ilianza bila mshambuliaji machachari wa klabu ya Crystal ya England Wilfried Zaha - waliutawala vyema mchezo huo katika kipindi cha kwanza na hakika walisikitika kwenda mapumziko bila kupata goli.
Hlatswayo aliikosesha Afrika Kusini ama Bafana Bafana goli la wazi kwa kupaisha kichwa krosi safi kutoka kwa Sifiso Hlanti.
Ivory Coast inayonolewa na Ibrahim Kamara itachuana na Morocco matika mchezo uaofuata wa Kundi D whuku Afrika Kusini ikipambana na Namibia, siku hiyohiyo.