Viongozi wa jeshi la Sudan wamesema kuwa wanafutilia mbali makubaliano yote yaliowekwa na upinzani na sasa wataandaa uchaguzi baada ya kipindi cha miezi tisa .
Tangazo hilo linajiri huku jeshi likikabiliwa na shutuma za kimataifa kuhusu jinsi linavyowashambulia waandamanaji katika mji mkuu wa Khartoum ambapo takriban watu 30 walifariki.
Marekani imesema kuwa lilikuwa shambulio la kikatili.
Msako huo ulianza baada ya jeshi na waandamanaji kukubaliana na serikali ya mpito ya miaka mitatu kabla ya raia kuchukua mamlaka.
Waandamanaji walihoji kwamba utawala uliopita wa rais Omar al-Bashir, ambaye alipinduliwa na jeshi mnamo mwezi Aprili baada ya miezi kadhaa ya maandamano umekita mizizi katika taifa hilo hivyobasi serikali ya mpito ya miaka mitatu inahitajika ili kuharibu mtandao wake wa kisiasa kwa lengo la kuruhusu uchaguzi wa haki.
Baraza la mpito TMC ambalo limekuwa likiongoza taifa hilo tangu mapinduzi pamoja na wawakilisha wa Vuguvu la kidemokrasia wamekubaliana kuhusu muundo wa utawala mpya.
Lakini mkuu wa baraza hilo jenerali Abdel Fatah al-Burhan alisema katika taarifa iliopeperushwa katika runinga ya taifa kwamba waliamua kuwacha majadiliano na muungano huo wa uhuru na mabadiliko na kufutilia mbali yale yote yaliokuwa yameafikiwa.
''Uchaguzi baada ya miezi tisa ,utafanyika chini ya usimamizi wa kieneo na ule wa kimataifa'' , aliongeza.
Akizungumza katika kipindi cha BBC News day , mchanganuzi na aliyekuwa balozi wa Uingereza nchini Sudan Rosalind Marsden alisema kuwa uchaguzi huo , utatoa fursa kwa idadi kubwa ya viongozi wa zamani kurudi mamlakani.
''Kuna hatari kubwa ya ghsia kuendelea'', alisema.
Kbla ya mauaji hayo , viongozi wa vuguvugu la kidemokrasia walisema kuwa wanafuta mawasiliano yote na baraza la mpito TMC na kutaka kufanyika kwa mgomo.
Serikali ya mpito
Jeshi la nchini Sudani limekemewa kutokana na mashambulizi yake dhidi ya waandamanaji mjini Khartoum, hatua iliyosababisha watu 30 kupoteza maisha.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka uchunguzi ufanyike akisema ametamaushwa na ripoti kuwa maafisa walifyatua risasi hospitalini.
Marekani na Uingereza zimesema ni ''tukio la kikatili''.
Sudan imekua chini ya utawala wa kijeshi tangu Rais Omar al-Bashir alipopinduliwa mwezi Aprili.
Viongozi walioongoza vuguvugu la kutaka utawala wa kiraia kuongoza nchi hiyo, wamesema wamesitisha mawasiliano na serikali ya mpito ya kijeshi na kufanya mgomo.
Vikosi vya usalama vilifika maeneo ambayo watu walikua wakiandamana, mapema Jumatatu na sauti za risasi zilisikika kwenye picha za video.
Katika taarifa yake iliyosomwa kwa njia ya televisheni ya taifa, Jeshi limeeleza masikitiko yake kwa namna hali inavyozidi kuwa mbaya na kusema kuwa operesheni ilikua imewalenga ''wanaotia dosari hali ya usalama na wahalifu''.
Jeshi limesema kuwa limekuwepo kwa ajili ya kulinda raia.
Awali, wanaharakati wamesema vikosi vya usalama waliizunguka hospitali moja mjini Khartoum na kufyatulia risasi hospitali nyingine.
Kamatikuu ya madaktari wa Sudan, walio karibu na waandamanaji wamesema watu 30 akiwemo mtoto wa miaka minane wa,meuawa, na idadi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka.
Baadhi ya wakazi wamekilaumu kikosi cha Rapid Support Forces, kilichokuwa kikipambana kumsaidia Bwana Bashur kubaki madarakani na kushiriki kwake kwenye mzozo wa Darfur magharibi mwa Sudan ulioanza mwaka 2003.
Wakati huo wakifahamika kwa jina ''Janjaweed'', wanamgambo hawa walitekeleza mauaji.
Nini kilifuata?
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka mamlaka za Sudan kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya wale waliohusika.
Taarifa yake imelaani matumizi ya nguvu kuwatawanya waandamanaji, na kushtushwa na ripoti kuwa vikosi vya usalama kufyatua risasi kwenye hospitali.
Shirika la habari la Sudan limesema mwendesha mashtaka ameunda kamatai kufanyia uchunguzi matukio hayo.
Ramadhan 'inavyoimarisha' maandamano Sudan
Waandamanaji wakata ushirikiano na jeshi Sudan
Chanzo ni nini?
Waandamanaji wamekua wakikita kambi nje ya jengo la makao makuu ya jeshi tangu tarehe 6 mwezi Aprili, siku tano kabla ya kuangushwa kwa utawala wa Bashir.
Mwezi uliopita, waandaaji na majenerali watawala walikubaliana kuhusu muundo wa serikali mpya na muda wa mpito wa miaka mitatu kuelekea kwenye utawala wa kiraia.
Hawajaweza kuamua kuhusu ni upande upi hasa kati ya raia au jeshi kuchukua nafasi nyingi zaidi.
|
0 Comments