Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, ACP. Jumanne Muliro akifungua kikao kazi cha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Dawati la Jinsia, Jeshi la Polisi na wataalamu wa afya mkoani Mwanza.


Kikao hicho kiliandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) la jijini Mwanza ili kuweka
mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana na
wahanga wa ukatili ikiwemo ubakaji na kutokomeza mimba katika umri mdogo.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji
wa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo
Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika la KIVULINI.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wanahabari wakinasa matukio kwenye warsha hiyo ya kikazi.
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifafanua jambo kwenye kikao hicho.
Mwakilishi kutoka jeshi la polisi mkoani Mwanza akiongoza wajumbe wa kikao kazi hicho kuweka mikakati ya upatikanaji wa huduma rafiki kwa wahanga wa ukatili.
Mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho akichangia mada.
Tazama BMG Online TV hapa chini