Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (katikati) akitoa salamu zake za shukrani baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika jana Juni 01, 2019 katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza kumchangua kushika nafasi hiyo hadi hapo mwakani 2020 uchaguzi mkuu utakapofanyika.
GB Pazzo, BMG
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) uliofanyika jana jumamosi Juni 01, 2019, wamewaondoa viongozi waliokuwa madarakani na kuwachagua viongozi wapya watakaokaa madarakani hadi mwakani 2020 utakapofanyika Uchaguzi/ Mkutano Mkuu.
Hatua hiyo ilijiri huku tayari tayari baadhi ya nafasi kama vile Mwenyekiti na Katibu Mkuu zikiwa wazi baada ya kujiuzulu mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu 2019 kufuatia mashinikizo kutoka kwa wanachama waliokuwa wakiwalalamikia kutotimiza vyema majukumu yao.
Katika uchaguzi huo, Edwin Soko alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti Albert Gsengo, Katibu Mkuu Magreth Kusekwa (akipanda kutoka Katibu Mkuu Msaidizi), Katibu Mkuu Msaidizi Projestus Binamungu, Mweka Hazina Paulina David (akitetea nafasi yake). Aidha mkutano huo pia uliwachagua wajumbe watano wa Kamati Tendaji MPC ambao ni George Binagi, Gloria Kiwia, Nashon Kennedy, Sitta Tuma pamoja na Philmon Malili (akitetea nafasi yake).
Itakumbukwa katika uchaguzi wa mwaka 2015, viongozi wa MPC waliochaguliwa walikuwa ni Mwenyekiti Osoro Nyawana (alijiuzulu), Makamu Mwenyekiti Neema Emmanuel, Katibu Mkuu Calvin Jilala (alijiuzulu), Katibu Mkuu Msaidi Magreth Kusekwa, Mweka Hazina Paulina David huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa ni Philmon
Malili, Martha Lume, Antony Gervas, Shagatta Suleiman (amehamia mkoani Simiyu kikazi) na Neema Mwita (ametangulia mbele za haki).
Malili, Martha Lume, Antony Gervas, Shagatta Suleiman (amehamia mkoani Simiyu kikazi) na Neema Mwita (ametangulia mbele za haki).
Viongozi hao walipaswa kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu lakini baadae UTPC ambayo ni taasisi inayolea klabu za waandishi wa habari Tanzania ilibadili Katiba na hivyo kufanya kupindi cha uongozi kwa klabu zote nchini kuwa miaka mitano badala ya mitatu.
Tazama picha na kisha video kujua zaidi yaliyojiri kwenye Mkutano Mkuu Maalum MPC
Makamu Mwenyekiti wa MPC, Albert George Sengo akisisitiza umoja na mshikamano baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Katibu Mkuu MPC, Magreth Kusekwa akitoa shukrani zake baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ambapo aliahidi ushirikiano ili kuhakikisha MPC inasonga mbele kimaendeleo.
Katibu Mkuu Msaidizi MPC, Projestus Binamungu akitoa salamu za shukrani ambapo alisisitiza uvumilivu miongozi mwa viongozi na wanachama kwa maslahi mapana ya chama.
Mweka Hazina MPC, Paulina David akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua kuitumikia tena nafasi hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Tendaji MPC yenye wajumbe wa watano akitoa salamu za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Nashin Kennedy akitoa salamu zake za shukrani.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Philmon Malili akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumuamini na kumchagua tena kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Sitta Tuma akitoa salamu zake za shukrani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mjumbe wa Kamati Tendaji MPC, Gloria Kiwia akiwashukru wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.
Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kwa kushirikiana na Hilda Kileo (hayuko pichani), akitoa ujumbe wako kwa wanachama na viongozi wapya MPC.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (katikati) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum MPC wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwa umakini.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti MPC, Deus Bugaywa (katikati) wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kwenye mkutano huo.
Viongozi wapia waliochagua kuiongoza MPC hadi hapo mwakani uchaguzi mkuu uakapofanyika kwa mujibu wa Katiba.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Wanachama wa MPC na viongozi wa UTPC wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya MPC.
Baadhi ya viongozi wapya MPC wakipongezana baada ya uchaguzi.
Maakuli pia yalikuwepo.
Tazama Video hapa chini
0 Comments