Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shia na mfanyabiashara, Azim Dewji, akiwa amelazwa hospitali ya Mchuki Mission, Kibiti.
MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Shia na mfanyabiashara, Azim Dewji, na waandishi watatu wa vituo vya televisheni vya ITV,  Channel Ten na Azam TV wamepata ajali jana, Julai 27, 2019, asubuhi baada ya gari lao kuacha njia wakati wakiwa njiani kuelekea Rufiji kwenye sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi mkubwa wa umeme wa MW 2,115 wa Rufiji mkoani Pwani.
Azim Dewji amelazwa kwa sasa hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi akipatiwa matibabu baada ya mfupa wake mmoja wa uti wa mgongo kuvunjika ajalini. Watu wote waliokuwa kwenye gari hilo wametoka salama.

Muonekano wa Gari ya Azim Dewji baada ya kupata ajali wakati akiwa njiani kuelekea Rufiji kwenye sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi mkubwa wa umeme wa MW 2,115 wa Rufiji mkoani Pwani.