Real Madrid wana imani watafanikiwa kumsajili kiugo wa kati Mfaransa Paul Pogba kutoka Manchester United msimu ujao. (ESPN)
Bayern Munich wameanza mazungumzo na Manchester City kuhusu usajiliwa wa winga wao wa miaka 23 Mjerumani Leroy Sane, amabaye thamani yake inakadiriwa kuwa £90m. (Mirror)
Romelu Lukaku, 26, amesafiri nyumbani Ubelgiji siku ya Ijumaa kufanya mazungumzo na ajenti wake huku Inter Milan wakikaribia kufikia mkataba wa £70m kumnunua kuingo huyo wa safu ya ushambulizi kutoka Manchester United. (Daily Mail)
Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley amesema chamsingi ni maishani ni "pesa kwanza kisha klabu baadae" kwa maneja wake wa zamani Rafael Benitez, na kuongeza kuwa "ni vigumu" kuendelea kumng'ang'ania raia huyo wa Uhispania. (Mail)
Atletico Madrid wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka kwa mahasimu wao Real Madrid. (Independent)
Mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 20, anajiandaa kuondoka Lille kwenda AC Milan kwa mkataba wa euro milioni 35 - utakaojumuisha 20% ya makataa ya kumuuza. (RMC Sport)
Bournemouth wanapania kuipiku Brighton katika usajili wa £15m wa kiungo wa kati wa Huddersfield Philip Billing, 23. (Sun)
Swansea City wanakabiliwa na hatari ya kumkosa mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 22-Kasey Palmer. (Wales Online)
Panathinaikos wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Ivory Coast anayechezea Celtic Kouassi Eboue, 21. (Daily Record)
Bekiwa Real Madrid wa miaka 22 Mhispania Jesus Vallejo anafanyiwa vipimo vya kimatibabu Wolves kabla ya kuhamia klabu hiyo kwa mkopo. (Talksport)
Tetesi Bora Ijumaa
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai kuwa wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na kusisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kilichopo badala ya kununua wachezaji wapya. (Independent)
Manchester United huenda ikalazimika kulipa Leicester City £80m kumnunua mlinzi wake Harry Maguire baada ya Eric Bailly kuumia goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham. (Mirror)
Mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele , 23, atakuwa katika urodha ya kujiunga na Manchester United klabu hiyo ikiamua kumuuza nyota wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, hana uwezo wa kumshawishi Neymar kujiunga na miamba wa Italia- kwa sababu nyota huyo wa Brazil wa miaka 27-ameamua kujiunga na Barcelona. (Star)
Borussia Dortmund wanafanya mazungumzo ya kumsajili mshambulizi wa Barcelona Malcom kwa euro milioni 42 (£37.5m). (Goal)
|
0 Comments