ASKARI wawili wa kanda maalum Rufiji, pamoja na Staff Officer I mkoa wa kipolisi Rufiji (ACP), Issah Bukuku, wanasemekana kufariki dunia katika ajali ya gari baada ya kupasuka gurudumu la nyuma na kupinduka na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wawili.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zinaeleza kuwa imetokea Julai 25 (jana) mwaka huu, huko kijiji cha Kilimahewa barabara ya Kilwa wilaya ya Mkuranga na mkoa wa kipolisi Rufiji ambapo gari namba PT. 3822 Toyota Land Cruiser mali ya jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Rufiji lilikuwa likiendeshwa na askari namba F7167 PC Ibrahim likitokea polisi Ikwiriri kuelekea kijiji cha Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.
Waliofariki dunia pamoja na Bukuku, ni Inspector Esteria wa ofisi ya RCO Rufiji na G 1132 PC Lameck wa FFU Rufiji.
Majeruhi katika ajali ni dereva wa gari hiyo F 7167 PC Ibrahim wa ofisi ya RCO Rufiji na G7651 PC Mgusi wa ofisi ya RPC Rufiji ambao wameumia sehemu mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na taarifa kamili za kipolisi kanda maalum Rufiji zinaendelea na uchunguzi na itatoa habari kamili.
0 Comments