SHEREHE za Siku ya Urembo wa Asili Tanzania mwaka huu zitafanyika wikiendi hii Jumamosi na Jumapili Julai 27, na 28 katika ukumbi wa Life Park Mwenge-Dar es Salaam, na hakuna kiingilio.
Kwa mujibu wa watayarishaji wa maonyesho hayo, kutatolewa mafunzo ya kutengeneza vipodozi vya asili na visivyo na kemikali bure, na kutakuwa na upimaji saratani ya matiti na elimu ya kansa aina mbalimbali, vyote hivyo vikifanywa bure.
Isitoshe, patatolewa kipaumbele kwa wanawake wajasiriamali wa kundi maalumu kama vile walemavu kushiriki katika maonyesho hayo ambapo watapewa banda bure la kuonyesha kazi zao pamoja na wajasiriamali vijana.
Kwa upande wa burudani, kutakuwepo malkia wa mipasho, Khadija Kopa, na mwimbaji Aneth Kushaba.
Pia kutakuwepo watu maarufu wakiwemo wasanii wa fani mbalimbali kama Mwasiti, Dina Marious, Grace Matata, Rose Ndauka na mchekeshaji Jaymond, ambapo watapata nafasi ya kuongea.
Burudani nyingine ni fasheni shoo kutoka kwa wasichana ‘naturalist’ na watoto.
0 Comments