Timu ya taifa wanawake ya Marekani ambayo leo hii imelitwaa kombe la dunia nchini Ufaransa baada ya kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Uholanzi kwa jumla ya goli 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika jiji la Lyon katika uwanja wa Parc Olympique Lyonnais nchini Ufaransa.
Marekani ndio nchi inayoendelea kulishikilia kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa mara ya mwisho mwaka 2015 baada ya kuifunga Japan mwaka huo 2015.
Wakicheza kwa kujihami kwa mashambulizi ya mfululizo kwa vipindi vyote viwili huku akiwatumia washambuliaji wake machachari Rose Lavelle na Megan Rapinoe ambao walionekana kuwa mwiba kwa timu ya taifa ya Uholanzi.
Bao la kwanza la Marekani lilifungwa kwa njia ya penati na mshambuliaji wa kushoto wa Marekani mwenye jezi namba 15 mgongoni kwa jina Megan Rapinoe baada ya mchezaji wao kuchezewa vibaya eneo la hatari.
Madada wa kiholanzi wakijitutumua japo walionyesha dhahiri kuelemewa kwa vipindi vyote viwili wakajikuta wanakubali bao la pili lililofungwa kwa shuti kali na mshambuliaji Rose Lavelle baada ya kuiadaa ngome ya Uholanzi na kumfanya golikipa wa timu ya taifa ya Uholanzi kushindwa kuzuia shuti hilo.Mpaka mwisho wa mchezo Marekani ikatoka uwanjani na kikombe kwa jumla ya goli 2-0.. |
0 Comments