Victor Wanyama
KIUNGO wa Harambee Stars na Tottenham Hotspurs ya Uingereza, Victor Wanyama amemkaribisha rasmi nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta katika Ligi Kuu ya England msimu ujao.

Kabla ya nyota huyo wa Spurs kumkaribisha Samatta katika ligi hiyo, tayari baadhi vyombo ya habari vikubwa
duniani vimeripoti kuwa nyota huyo anatakiwa na Leicester City, Middlesbrough na Aston Villa huku dau lake likiwa Sh Bil 34 za Kibongo.

Samatta anayekipiga katika KRC Genk ambayo msimu uliopitia alifungia mabao 32 katika michuano yote huku akifanikiwa kushinda kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora ndani ya timu yake.

Samatta ambaye tayari ameshaweka wazi kuwa hatarajii kuendelea kucheza Ubelgiji msimu ujao, alitumia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kuandika kuwa: “Ilikuwa ni nafasi nzuri kucheza na mmoja wa wachezaji bora na wa mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, tunajivunia uwepo wako ndani ya East Africa (Afrika Mashariki).”

Kabla ya Wanyama kujibu post ya Samatta kwa kumkaribisha kwenye ligi hiyo maarufu duniani kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Twitter kwa kuandika matarajio yake ni kumuona mshambuliaji huyo kwenye ligi hiyo msimu ujao.

“Nashukuru sana kaka yangu, na ni matarajio yangu kukuona Premier League msimu ujao tuendelee kupeperusha bendera ya East Africa.”

Samatta na Wanyama walikutana katika michuano ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ inayoendelea nchini Misri wakiwa kundi moja kabla ya wote kutolewa kwenye makundi.